BABA LEVO KUTUMIA MABANGO YA KAMPENI KUTENGENEZA MEZA ZA WAFANYABIASHARA KIGOMA MJINI
Na Hamida Ramadhan, Dodoma. MBUNGE wa Kigoma Mjini Mheshimiwa Clayton Revocatus Chipando anayejulikana kwa jina la Baba Levo ameonyesha mfano wa ubunifu na uwajibikaji kwa kutumia mabango 80000 ya kampeni yaliyosalia baada ya uchaguzi kutengeneza meza zitakazotolewa bure kwa wafanyabiashara wadogo katika masoko ya Kigoma Mjini. Akizungumza na waandishi wa habari mbunge huyo Baba Levo amesema hatua hiyo inalenga kuboresha mazingira ya wafanyabiashara na kuonyesha kwamba hata vifaa vilivyotumika kisiasa vinaweza kuwa na faida kijamii endapo vitatumiwa kwa ubunifu. Amesema badala ya mabango ya kampeni kubaki yakiharibu mazingira wameamua kuyageuza kuwa meza imara kwa ajili ya wafanyabiashara wa Kigoma ni njia ya kugeuza alama za siasa kuwa alama za maendeleo. Meza hizo zitatolewa rasmi wiki ijayo katika mkutano mkubwa wa shukurani utakaofanyika Kigoma Mjini ambapo Baba Levo atawashukuru wananchi kwa imani waliyoonyesha kwake na kueleza mwelekeo wa uongozi wake mpya. "Mpango wa kutu...