Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari 11, 2026

TANZANIA YANG'ARA DUNIANI KUNDI LA VINARA WA SERIKALI KIDIGITALI - WORLD BANK 2025.

Picha
Na Hamida Ramadhani. TANZANIA imeendelea kung’ara kimataifa baada ya Benki ya Dunia (World Bank – WB) kuitaja kuwa miongoni mwa nchi zilizo na ukomavu wa juu wa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika sekta ya umma.  Hatua hii ni uthibitisho wa mafanikio ya mageuzi ya kidijitali yanayoendelea kutekelezwa na Serikali katika kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi. Kwa mujibu wa Ripoti ya GovTech Maturity Index (GTMI) ya mwaka 2025, Tanzania imeorodheshwa katika Kundi A – Ukomavu wa Juu wa Matumizi ya TEHAMA (Extensive GovTech Maturity).  Kundi hili linajumuisha nchi zinazoongoza duniani katika matumizi ya teknolojia katika utoaji wa huduma za serikali na ushirikishwaji wa wananchi kidijitali. GTMI: Kipimo cha Ukomavu wa Serikali Kidijitali. Ripoti ya GTMI hutathmini ukomavu wa matumizi ya TEHAMA serikalini katika takriban nchi zote duniani, ikizingatia maeneo muhimu kama sera, sheria, miongozo, mifumo ya TEHAMA na utekelezaji wake. Toleo la 2025 la ripot...

MIRERANI WALIA NA MAJI YA KUNYWA

Picha
  Na Mwandishi wetu, Mirerani. WAKAZI wa mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara, kwa zaidi ya wiki moja wamelalamikia kutopata huduma ya maji ya kunywa, baada ya malori yanayouza maji hayo kutoka mji mdogo wa Boma ng'ombe wilayani Hai mkoani Kilimanjaro kudaiwa kuzuiwa. Kwa zaidi ya miaka 20 wakazi wa mji mdogo wa Mirerani, wanatumia maji ya kunywa yanayouzwa na malori kutoka mji mdogo wa Boma ng'ombe. Hivi sasa, baadhi ya wakazi wengine wa mji huo wanatumia maji ya visima vifupi na virefu na maji ya mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jiji la Arusha (AUWSA) Mirerani, kwa ajili ya matumizi mengine ikiwemo kunywa. Baadhi ya wakazi wa mji mdogo wa Mirerani, wakizungumza juu ya changamoto hiyo wameiomba serikali kuingilia kati suala hilo kwani wanatumia gharama kubwa kupata maji ya kunywa. Mmoja kati ya wakazi hao, Andrew John amesema kwa zaidi ya miaka 20 walikuwa wanatumia maji ya kunywa yanayotoka Hai ila wanasikitishwa hivi sasa kupata zuio hilo. "...

JAMII YASWA KUWAPA NAFASI SAWA WATU WENYE ULEMAVU KATIKA ELIMU YA DINI.

Picha
  Na Hamida Ramadhan, Dodoma. SHEIKH wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajab, ameitaka jamii kuacha tabia ya kuwatenga watu wenye Ulemavu na badala yake kuwapa nafasi sawa, hususan katika elimu na masuala ya dini, kwani nao ni sehemu muhimu ya jamii na wana haki sawa ya kujifunza na kutekeleza mafundisho ya dini. Sheikh Rajab ameyasema hayo alipo hutubia katika Mashindano ya Kitaifa ya Kuhifadhi Qur’an Tukufu kwa Watu wenye Ulemavu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Riziki Lulida Foundation. Amesema kuwa, mashindano hayo ni ya kipekee kwa kuwa yanawaleta pamoja kundi la watu ambalo kwa muda mrefu limekuwa likisahaulika na kupuuzwa na jamii. " Kwa miaka mingi jamii imekuwa ikiwanyima watu wenye ulemavu fursa mbalimbali bila kutambua kuwa nao ni binadamu kamili wenye haki ya kusoma, kuabudu na kushiriki kikamilifu katika masuala ya dini," amesema Sheikh Rajab. Ameongeza kuwa, kupitia mashindano hayo hatua muhimu imechukuliwa kurejesha heshima, thamani na nafasi yao katika jamii. Aidha, Shei...

SELWA :- ATOA ONYO KALI KWA WASIMAMIZI WA MIRADI IGUNGA.

Picha
  Na Lubango Mleka, Igunga. MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Selwa Hamid amewataka Wasimamizi wa Mafundi na Kamati za ujenzi kusimama  katika nafasi zao kwa lengo la kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa wakati na kuzingatia viwango vya fedha. Selwa ametoa wito huo, wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali katika kata za Jimbo la Manonga wilayani Igunga. "Tujirekebishe kwenye miradi yetu na kuongeza usimamizi kwa sababu hali ya  mafundi kuondoka maeneo ya ujenzi wakati unaendelea  hatukubaliani nayo," amesisitiza na kuongeza kuwa, "Ziogopeni fedha hizi za miradi kama ukoma na mambo ya udalali yasiwepo kwenye miradi, wapeni mafundi wanaofanya kazi ipasavyo."