Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai 24, 2025

RAIS MWINYI AWASILI JIJINI DODOMA

Picha
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameondoka Zanzibar na kuwasili Jijini Dodoma kushiriki kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yatakayofanyika katika Uwanja wa Mnara wa Mashujaa uliopo Mji wa Serikali-Mtumba Dodoma, siku ya Ijumaa tarehe 25 Julai , 2025. Katika Uwanja wa ndege wa Dodoma, Rais Dkt.Mwinyi amepokelewa na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Mkoa huo.

DARAJA LA MSANGI KUFUNGUA MAWASILIANO VIJIJI VYA IRAMBA.

Picha
Na Mwandishi Wetu, ramba - Singida KUKAMILIKA kwa daraja la Masagi linalojengwa katika barabara ya Kibirigi-Masagi kutasaidia kuunganisha vijiji vya Kibirigi, Masagi na Tyeme katika Kata ya Mtoa, Wilaya ya Iramba mkoani Singida.  Hayo yameelezwa na Meneja wa TARURA Mkoa wa Singida Mhandisi Ibrahim Kibasa wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mradi huo mbele ya Kamati ya Ukaguzi ya TARURA inayofanya ziara ya Ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa Miundombinu ya barabara mkoani humo. "Vijiji vya Kibirigi, Masagi na Tyeme vinajishughulisha na shughuli za kilimo hususani pamba, alizeti, dengu, mahindi pamoja na ufugaji, hivyo kukosekana kwa daraja katika Mto sekenke linapojengwa daraja hilo ilikuwa ni kikwazo kwao katika kuyafikia masoko ya mazao yao na kurudisha nyuma jitihada za kujiletea maendeleo". amefafanua Mhandisi Kibasa.  Kwa mujibu wa Mhandisi Kibasa kukamilika kwa Mradi huo utachochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika vijiji hivyo na kuchangia ustawi wa maendeleo ya Wi...

TCRA YATOA ELIMU KUHUSU MATUMIZI SAHIHI YA HUDUMA ZA MAWASILIANO

Picha
Afisa Mhifadhi Mwandamizi - TCRA Bw. Raphael Mwango akitoa elimu kuhusu matumizi sahihi na salama ya huduma za mawasiliano ikiwemo mitandao katika kituo cha redio cha Hatma FM, kipindi Maalumu jana tarehe 23, Julai, 2025 Arusha.  TCRA imeleta tena kampeni nyingine ya elimu kwa umma yenye jina la “FUTADELETEKABISA” ikiendelea kusisitiza matumizi sahihi na salama ya huduma za mawasiliano na kukumbusha wajibu wa watumiaji wa kusambaza taarifa za ukweli na uhakika na kufuta na kutosambaza ujumbe au taarifa zinazochochea upotoshaji, uzushi, chuki na uvunjifu wa amani.

TIMU YA WANAWAKE YA MPIRA WA PETE YA KVZ YANYAKUA KOMBE.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.  TIMU ya wanawake KVZ Netball Club imefanikiwa kuibuka na ubingwa wa kombe la ligi kuu ya zanzibar kwenye mashindano yaliyofanyika kisiwani Pemba mwaka huu 2025 KVZ Netball Club inaendelea kuweka historia ya kuchukua ubingwa huo mara tano mfululizo tangu kuanzishwa kwake. Aidha, Pongezi nyingi zimemuendea kamanda mkuu wa kikosi cha Valantia Zanzibar Lt. Col Luteni Kanali Said Ali Shamhuna kwa kuwa bega kwa bega na timu hiyo kuhakikisha inafanya vizuri katika kila mashindano ambayo inashiriki. Ikumbukwe kwa sasa kvz Netball Club ni mabingwa wa jumla kwa Tanzania nzima.

WANANCHI WAHIMIZWA KULINDA MIUNDOMBINU YA ELIMU IRINGA.

Picha
Na Mwandishi Wetu. MKUU wa Mkoa wa Iringa Mhe. Kheri James kwa kutambua kazi iliyofanywa na serikali amewahimiza Wananchi mkoani humo kuhakikisha wanalinda na kuitunza miundombinu iliyojengwa katika sekta ya elimu mkoani humo ili iweze kutumika kwa muda mrefu na kuufikisha mkoa katika lengo la kuinufaisha jamii kielimu na taifa kwa ujumla. Ametoa rai hiyo wakati akizungumzia hatua zilizofikiwa na maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya elimu kupitia Mradi wa kuimarisha Ubora wa Elimu ya Sekondari nchini (SEQUIP). Mhe Kheri amesema kuwa Mkoa wa Iringa katika kipindi cha miaka mitano ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanzia mwaka 2020 hadi 2025 umepokea kiasi cha shilingi 21,017,700,420.  Amesema fedha hizo zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya Shule za Sekondari. Aidha, miundombinu iliyojengwa katika kipindi hicho ni pamoja na Shule mpya za kata, Shule ya wasichana ya Mkoa (Lugalo), Shule ya amali Mafinga, Mabweni, Madarasa, nyumba za walimu pamoja na ma...

BIL 36.596 ZA MRADI WA SEQUIP ZILIVYO INUFAISHA DODOMA KWENYE SEKTA YA ELIMU.

Picha
  BIL 36.596 ZA MRADI WA SEQUIP ZILIVYO INUFAISHA DODOMA KWENYE SEKTA YA ELIMU.  Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  MKOA wa Dodoma ni miongoni mwa maeneo ambayo yamepata fedha nyingi kupitia mradi wa kuimarisha ubora wa Elimu ya sekondari nchini SEQUIP ambapo umepokea zaidi ya Bilioni 36.596 Fedha hizo ambazo zimetolewa na serikali zimetumika kujenga shule mpya 41 za Sekondari ambazo miongoni mwake ni pamoja na Shule 1 ya wasichana, Shule 1 ya kanda ya Wavulana, Shule za kata 36, Shule 1 ya Amali ya Mkoa, na Shule 2 za Amali za kata. Hayo yamebainishwa na Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma Mwl Vicent Kayombo ambapo amesema kuwa fedha hizo pia zimetumika kujenga Madarasa 77, Matundu ya Vyoo 119, Maabara 19, Mabweni 22, na Nyumba za Walimu 22. Mwl Kayombo amesema kuwa mkoa wa Dodoma umejenga shule mpya ya wasichana Manchali kwa gharama ya Shilingi Bilioni 4.450 sambamba na ujenzi wa shule mpya ya Amali ya mkoa iliyojengwa katika kijiji cha Manchali wilayani Chamwino kwa gharama ya Shiling...