TIMU YA WANAWAKE YA MPIRA WA PETE YA KVZ YANYAKUA KOMBE.

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar. 

TIMU ya wanawake KVZ Netball Club imefanikiwa kuibuka na ubingwa wa kombe la ligi kuu ya zanzibar kwenye mashindano yaliyofanyika kisiwani Pemba mwaka huu 2025

KVZ Netball Club inaendelea kuweka historia ya kuchukua ubingwa huo mara tano mfululizo tangu kuanzishwa kwake.

Aidha, Pongezi nyingi zimemuendea kamanda mkuu wa kikosi cha Valantia Zanzibar Lt. Col Luteni Kanali Said Ali Shamhuna kwa kuwa bega kwa bega na timu hiyo kuhakikisha inafanya vizuri katika kila mashindano ambayo inashiriki.

Ikumbukwe kwa sasa kvz Netball Club ni mabingwa wa jumla kwa Tanzania nzima.





Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.