Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari 29, 2026

MJI ULIOPO CHINI YA ARDHI WAGUNDULIWA SYRIA

Picha
  “Mji uliopo chini ya ardhi” wenye ghorofa tatu uligunduliwa tarehe 27 Januari mwaka 2026 nchini Syria. Mji huo ulijengwa na Jeshi la Kidemokrasia la Syria (SDF) chini ya mlima katika mji wa Sirrin, ambao ni sehemu ya eneo la Ayn al-Arab na unaunganishwa na mahandaki mengi.

DKT. KIJAJI AMWAPISHA CC BADRU NA KUZINDUA BODI YA NGORONGORO

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Arusha KAMISHNA Uhifadhi wa  Mamlaka ya Ngorongoro   Abdul - Razaq  Badru ametakiwa kuhakikisha hifadhi ya Ngorongoro inalindwa na kuhifadhiwa ili ikolojia yake istawi na kuendelea kuvutia watalii,kuhifadhi wanyamapori, misitu na viumbe hai wengine.  Hayo yamesemwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, jijini Arusha baada ya kumwapisha Kamishna huyo na kuizindua Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Dkt. Kijaji amesema kuwa, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ameonesha imani kubwa kwa Kamishna huyo, hivyo pamoja na mambo mengine anapaswa kuingoza vyema Mamlaka hiyo ili iweze kufikia matarajio yaliyokusudiwa hususani ya kufikia ya idadi ya watalii Milioni 8 kitaifa.  "Unapaswa uhakikishe huduma za malazi zinaendelea kuboreshwa kwa kuvutia uwekezaji  utakaoongeza vitanda  kutoka  1,555  hadi kufikia vitanda 2,586". Alisema Dkt. Kijaji. Ame...

BUNGE BONANZA: WASHIRIKI WATAJITOELEA KUCHANGIA DAMU SALAMA

Picha
  Na Hamida Ramadhan, Dodoma. MWENYEKITI  wa Bunge Bonanza, Festo Sanga, amesema washiriki wa Bunge Bonanza wanatarajiwa kujitolea kuchangia damu salama kwa hiari katika tukio litakalofanyika Jumamosi, Januari 31, 2026, kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari John Merlin Miyuji jijini Dodoma. Akiongea na waandishi wa habari  leo Januari 29 ,2026 Bungeni jijini Dodoma Sanga amesema zoezi hilo lina lengo la kuokoa maisha ya wagonjwa, kupunguza dharura za kiafya na kuimarisha mshikamano wa kijamii kati ya washiriki na jamii kwa ujumla. Ameeleza kuwa kuchangia damu ni kitendo cha huruma kinachoongeza uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa afya na mshikamano wa kitaifa. Amesema Bunge Bonanza linahusisha mashindano ya michezo ya burudani ikiwemo mpira wa miguu, kuruka kamba, pete, mashindano ya kula, kufukuza kuku pamoja na michezo mingine yenye lengo la burudani na mshikamano. Ameongeza kuwa tukio hilo litawakutanisha mashabiki wa timu za soka za Simba na Yanga, washiriki kutoka vyuo...

TANZANIA NA BRAZIL ZAAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dodoma. TANAZANIA na Brazil zimeahidi kuendelea kushirikiana katika sekta za kimkakati zenye maslahi mapana kwa mataifa haya mawili ikiwemo Afya, Kilimo, biashara, uwekezaji, elimu na ulinzi na usalama. Hayo yamebainishwa wakati wa mazungumzo baina ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe na Balozi wa Brazil nchini Mhe. Gustavo Martins Nogueira yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma Januari 29, 2026.  Viongozi hao wamejadili  masuala kuhusu ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Brazil kwa kipindi cha miongo mitano iliyopita na kukubaliana kuendelea kuuimarisha ushirikiano huo na kuupeleka katika viwango vya juu ili kuwawezesha wananchi kunufaika nao. Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Maghembe aliishukuru Serikali ya Brazil kwa kusaidia utekelezaji wa miradi ya zao la pamba ya Beyond Cotton na Cotton Victoria na kusistiza umuhimu wa kuibua miradi mingine zaidi.  “Miradi hii imejik...

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI

Picha
 

POLISI NJOMBE WAKANUSHA TAARIFA ZA ASKARI KUCHOMWA MOTO NA KUPORWA SILAHA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Njombe. JESHI la Polisi Mkoa wa Njombe katika taarifa yake kwa Vyombo vya habari limekanusha taarifa zilizokuwa zimesambazwa katika Mitandao ya Kijamii nchini zikiambatana na picha mjongeo (Video), zikieleza uwepo wa Askari Polisi wa Mkoa huo aliyechomwa moto na kisha kuporwa silaha Mkoani humo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Mahamoud Banga, Januari 28, 2026 amesema kuwa katika Mkoa wa Njombe hakuna tukio kama hilo, akionya dhidi ya wanaoandaa na kusambaza taarifa za uongo na upotoshaji. "Jeshi la Polisi linatoa wito kwa baadhi ya wananchi wenye tabia za kuandaa na kusambaza taarifa za uongo na upotoshaji kwa njia mbalimbali kuacha kwani ni kinyume cha sheria za nchi na maadili ya Mtanzania na hakuna faida yoyote kwa wanaofanya hivyo pamoja na familia zao na kwa jamii kwa ujumla." Amesema Kamanda Banga. Polisi pia imesema inaendelea kumfuatilia mtu ama watu waliochukua na kutumia picha mjongeo ya tukio la zamani ambalo as...

MWANACHAMA WA CHADEMA ARUSHA MATATANI KWA KUIBA 'FEDHA ZA LISSU

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Arusha. JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha limetangaza kumkamata Bw. Fredrick Mbwambo, Mwanachama wa Chadema na Mkazi wa Arusha kwa tuhuma za wizi wa fedha ambazo alikuwa amezikusanya kutoka kwa wananchi waliokuwa wamechanga kwaajili ya Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Tundu Lissu kupitia Kampeni yao ya "Funga mwaka na Tundu Lissu". Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Justine Masejo leo Jumatano Januari 28, 2026 Jijini Arusha mbele ya wanahabari, amesema ukamataji wa mtuhumiwa huyo umefanyika baada ya Polisi kupokea malalamiko kutoka kwa Bw. Alute Mughwai, aliyeeleza kubaini wizi wa fedha zilizokuwa zimechangwa. "Ufuatiliaji wa awali umeonesha kuwa ukusanyaji huo wa fedha ulikuwa ukifanywa kupitia namba mbili za simu za makampuni tofauti ya simu na inadaiwa zilihamishwa kwenye namba mbili za simu, moja ikiwa ni ya kampuni ya Tanzania na ya pili ikiwa ni ya kampuni ya simu ya nchi jirani." Amesema Kamanda Masejo...

KUSUASUA KWA UJENZI WA BARABARA MOSHI VIJIJINI: MBUNGE MAKOI AZUNGUMZA NA WAZIRI WA UJENZI

Picha
  Na Hamida Ramadhan,  Dodoma LICHA ya Serikali ya awamu ya sita kuendelea kujenga Miundombinu Mizuri ya Barabara hapa nchini, Mbunge wa Jimbo la Moshi vijiji Mhe. Morris Makoi amekutana na kufanya Mazungumzo na Waziri wa Ujenzi Mhe. Abdallah Ulega kuhusiana na Kusuasua kwa Miradi ya ujenzi katika Jimbo hilo. Mhe. Makoyi ametaja barabara hizo ikiwemo barabara ya Rau Madukani- Mamboleo Materuni yenye urefu wa kilomita 9.99 ambapo urefu uliokamilika ni 2.9. Akizungumza na Waziri wa Ujenzi Mhe. Ulega Mara baada ya kukutana na Kufanya Mazungumzo Mhe. Makoi amesema barabara hizo zimekuwa changamoto hivyo ni vyema serikali ikafanya mchakato kukamilisha ujenzi ili wananchi wapate Kutumia barabaraza hizo. "Barabara ya chekereni-Kahe- Mabogini yenye urefu wa kilomita 31.25, kiboriloni- Mbokomu kilomita 14.34, Moshi International school- kibosho kati-Raphael kilomita 13.9, Samanga Chemchem kilomita 9.91, Mamboleo Shimbwe kilomita 10.3 pamoja na barabara ya Kidia road(usuduni-Kidia) kilo...

DKT.JAFO AIBANA WIZARA YA UJEZNI,BARABARA YA LAMI MLANDIZI-MZENGA-BOGA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dodoma. MBUNGE wa Jimbo la  Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo, amehoji mpango wa Serikali wa kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya ujenzi wa Barabara ya Mlandizi–Mzenga–Maneromango kwa kiwango cha lami, akisisitiza kuwa ni barabara muhimu kwa shughuli za kiuchumi na kijamii. Akiuliza swali la nyongeza Bungeni, Dkt. Jafo amesema barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 70.2 inaanzia Mlandizi kupitia Mzenga hadi Maneromango, na kwamba tayari upembuzi yakinifu umekamilika. Ameeleza kuwa kwa sasa mkandarasi ameanza kazi katika kipande cha Mzenga chenye urefu wa mita 300, hali iliyomfanya kuihoji Serikali kuhusu mpango wake wa kuongeza fedha katika bajeti ya mwaka huu ili kufungua kipande cha Mlandizi hadi Mzenga. “Nini mpango wa Serikali katika bajeti ya mwaka huu kuongeza fedha ili kuhakikisha barabara hii muhimu inaanza kujengwa kuanzia Mlandizi hadi Mzenga?” amehoji Dkt. Jafo. Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, amesema Serikali...