Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili 29, 2026

TAMASHA LA KILIMO LAHITIMISHWA MBEYA

Picha
REA Yapongezwa uhamasishaji matumizi ya nishati safi ya kupikia, Umeme sasa ni kitongoji kwa kitongoji.  Na Mwandishi Wetu, Iwambi - Mbeya.  TAMASHA  la Kilimo lililofanyika mkoani Mbeya limehitimishwa rasmi leo Jumatano, tarehe 29 Aprili 2026, kwa mafanikio makubwa huku likiwa limekusanya wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo, nishati na maendeleo kutoka ndani na nje ya mkoa huo.  Tamasha hilo limekuwa jukwaa muhimu la kubadilishana uzoefu, kuonesha teknolojia mpya na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu njia bora za kuboresha maisha yao kupitia kilimo na matumizi sahihi ya nishati. Akizungumza wakati wa hafla ya kufunga tamasha hilo,mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Rungwe Mhe. Jaffar Haniu ameipongeza REA kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya matumizi ya nishati safi, akisisitiza kuwa hatua hiyo ina mchango mkubwa katika kuboresha afya za wananchi na kulinda mazingira.  Alieleza kuwa matumizi ya nishati safi kama majiko ya umeme, majiko y...

AAPAM KUKUTANISHA WATAALAM JIJINI ARUSHA ILI KUJADILI NAMNA YA KUIMARISHA UTAWALA BORA NA KUONGEZA UFANISI KATIKA UTOAJI HUDUMA KWA WANANCHI

Picha
  Na Hamida Ramadhan, Dodoma.  WATAALAMU wa Utawala wa umma na usimamizi wa rasilimaliwatu nchini wanatarajiwa kukutana jijini Arusha kuanzia Mei 5 hadi 8, 2026 katika Mkutano Mkuu wa Pili wa mwaka wa Jumuiya ya Wataalamu wa Utawala wa Umma na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Barani Afrika (AAPAM) Tawi la Tanzania. Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa AAPAM Tanzania Chapter, Leila Mavika, amesema mkutano huo utafanyika jijini Arusha ukiwaleta pamoja wataalamu wa kada hiyo ili kujadili namna ya kuimarisha utawala bora na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi. Kwa mujibu wa  Mavika, mkutano huo unalenga kutoa fursa ya kubadilishana uzoefu, kujadili changamoto zinazowakabili katika utendaji kazi na kubaini fursa za kuboresha usimamizi wa rasilimaliwatu na utawala katika utumishi wa umma. Ameongeza kuwa mkutano huo utaongozwa na wataalamu wabobezi watakaowasilisha mada mbalimbali za kitaaluma zitakazochochea maboresho ya utendaji na kuongeza tija katik...

DC MWEMA AONGOZA ZOEZI LA UTEKETEZAJI BANGI KITETO

Picha
  Na Hamida Ramadhan, Kiteto - Manyara.  MKUU wa Wilaya ya Kiteto Mheshimiwa Remidius Mwema ameongoza zoezi la uchomaji ekari tano za dawa za kulevya aina ya bangi iliyolimwa ndani ya mashamba ya mahindi katika kitongoji cha Kimaraunga, Kijiji cha Mbigiri Kata ya Partimbo. Mhe DC Mwema amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano  kwa Serikali kukabiliana  na ulimaji wa bangi huku akipongeza jitihada za utoaji taarifa zinazosaidia kubaini uwepo wa mashamba hayo.  Amelitaka jeshi la polisi kuhakikisha linawakamata watuhumiwa wote ikiwa ni pamoja na wamiliki wa mashamba hayo huku akisisitiza wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ili sheria ichukue mkondo wake. “Tumeshirikisha wananchi katika zoezi la kuteketeza dawa za kulevya ili kuonyesha kwa vitendo dhamira njema ya Serikali katika mapambano haya na tunatuma ujumbe kwa wananchi wote kuendelea kukabiliana na hali hii, operesheni hizi zitaendelea wakati wote ndani ya Wilaya yetu ,wananchi waendele...

DOLA BILIONI 1.3 KUJENGA SGR KIPANDE CHA MAKUTUPORA -ISAKA

Picha
  Na Lubango Mleka, Dodoma.  SERIKALI imeandika historia mpya katika sekta ya uchukuzi baada ya kusainiwa  mkataba wa Dola za Marekani Bilioni 1.277 kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Reli ya Kisasa ya Standard Gauge Railway (SGR) Lot 3 na 4 kutoka Makutupora hadi Isaka kilometa 368 na Tabora mpaka Isaka 165 na kufanya jumla ya kilometa 533, utiaji Saini huo umefenyika leo tarehe 28 Aprili, 2026  katika  Ukumbi wa Treasury Square jijini Dodoma. Zoezi la utiaji Saini huo  lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Taasisi za kifedha, mabalozi pamoja na wadau wa maendeleo, huku Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Dkt. Khamis Mussa Omar, akiwa mgeni rasmi. Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Omar amesema jumla ya mashirika 3 ya fedha kutoka nchi za Italy, Sweden na Poland yamefadhili  jumla ya dola  Bil. 1.277 kwa ajili ya kuendeleza kipande hicho ambacho utekelezaji wake ulishaanza. Amesema huu ni uendelezaji wa ujenzi wa Reli hii ya kisasa kwa ku...

ZAO LA CHOROKO LALETA NEEMA KWA WAKULIMA TABORA

Picha
  Na Allan Kitwe, Tabora.  CHAMA Kikuu cha Ushirika wa Wakulima (IGEMBEMBENSABO) kimeeleza kufurahishwa na mafanikio makubwa waliyopata wakulima wa zao la choroko na mazao mengine katika msimu uliopita na matarajio yao makubwa msimu huu. Meneja Mkuu wa Chama hicho kinachosimamia wakulima wa Wilaya za Igunga na Nzega, Baraka Samwel Kiboye ameeleza kuwa mafanikio hayo yamechochewa na kazi nzuri inayofanywa na serikali ya Awamu ya Sita kuinua sekta ya kilimo. Ameeleza kuwa katika msimu uliopita wakulima walizalisha jumla ya tani 1,800 za choroko kati ya makisio ya tani 2,000 na kuziuza kwa bei ya sh 1,500 kwa kilo kwa mfumo wa stakabadhi ghalani tofauti na ile ya kawaidia ya sh 800 hadi 1000. "Baada ya mauzo wakulima walilipwa zaidi ya shilingi bilioni 2.7 na zote ziliingia katika mifuko yao, haya ni mafanikio makubwa sana, na mwaka huu tunatarajia kupata kilo nyingi zaidi na zote zitauzwa kwa mfumo huo huo", amesema.  Kiboye ameongeza kuwa pia wameanzisha utaratibu wa wakul...