Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni 23, 2026

DG TASAC: KUKAMILIKA KWA MV LIEMBA KUTAIMARISHA BIASHARA, USAFIRI NA UCHUMI KIGOMA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Kigoma.  MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Bw. Mohamed Salum, amesema kukamilika kwa ukarabati wa meli ya MV Liemba kutaimarisha huduma za usafiri wa majini, kuchochea biashara na kuharakisha maendeleo ya uchumi wa Mkoa wa Kigoma na ukanda mzima wa Ziwa Tanganyika. Bw. Salum amesema hayo leo, tarehe 23 Juni, 2026 alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa meli hiyo katika Bandari ya Kigoma, ikiwa ni sehemu ya shughuli za Maadhimisho ya 16 ya Siku ya Mabaharia Duniani yanayoendelea mkoani humo. Amesema wananchi wanaoishi katika maeneo yanayozunguka Ziwa Tanganyika wanategemea kwa kiwango kikubwa usafiri wa majini kwa shughuli za biashara, usafirishaji wa bidhaa na huduma za kijamii, hivyo kukamilika kwa MV Liemba kutaboresha huduma hizo na kuongeza ufanisi wa usafiri salama na wa uhakika. "MV Liemba ni meli yenye umuhimu mkubwa kwa wananchi wa ukanda wa Ziwa Tanganyika. Kukamilika kwake kutaimarisha usafiri salama, k...

RC MTANDA: ONGEZENI MAPATO, FUTENI HOJA ZA CAG

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Mwanza.  MKUU wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameutaka Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema kuongeza juhudi katika ukusanyaji wa mapato ya ndani ili kuimarisha utoaji wa huduma na kuhakikisha halmashauri inapata uwezo wa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Mhe. Mtanda ametoa kauli hiyo wakati akizungumza katika Mkutano wa Baraza Maalumu la kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), amesisitiza kuwa mapato ndiyo msingi wa uendeshaji wa halmashauri na huwezesha watumishi na madiwani kupata stahiki zao kwa wakati. Aidha, ameutaka Uongozi wa Halmashauri kusimamia kikamilifu miradi ya maendeleo ili kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana na wananchi wanapata manufaa yaliyokusudiwa kupitia miradi inayotekelezwa katika maeneo yao. Kuhusu maagizo ya Kamati za Bunge, RC Mtanda amesema Halmashauri inapaswa kuandaa taarifa za kina kuhusu utekelezaji wa maelekezo hayo badala ya kutoa taarifa za jumla zisizoonyesha hatua zilizo...

RC MTANDA AKABIDHI PIKIPIKI 18 KWA VIKUNDI 2 VYA VIJANA BUCHOSA

Picha
Na Mwandishi Wetu, Mwanza.  MKUU wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo tarehe 23 Juni, 2026 amekabidhi pikipiki 18 zenye thamani ya Tshs. Milioni 54.9 vya vikundi viwili vya vijana vya Bodaboda Lugasa na Waungwana Group Mbugani. Akiongea kwenye hafla ya makabidhiano hayo Mhe. Mtanda ameipongeza halmashauri hiyo kwa kuendelea kufanya vizuri kwenye eneo la matumizi ya fedha za mapato ya ndani kwa maendeleo ya wananchi. Halmashauri ya Buchosa inafanya vizuri sana , kwanza kwenye kukusanya mapato na pili kwenye kutumia kwa ajili ya maendeleo ya wananchi kwa kutumia mapato yao kununua vyombo kama pikipiki na kukopesha kwa vijana. Amesema Mkuu wa Mkoa. Aidha, ametoa wito kwa halmashauri hiyo kusimamia urejeshaji wa mikopo hiyo ili itumike kununua zingine na kuwezesha makundi mengine yaweze kukopeshwa. Aidha, amewataka vijana walionufailka na mkopo huo kuheshimu sheria za usalama barabarani kwa kuendesha kwa staha kwa usalama wao na wa watumia barabara wengine aidha kuzitumia pia kwa mal...

NIMERIDHIKA NA MATUMIZI MAZURI YA FEDHA ZA HALMASHAURI - RC MTANDA

Picha
Na Mwandishi Wetu, Mwanza.  MKUU wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewapongeza Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa kwa kufikia malengo kwenye ukusanyaji na matumizi mazuri ya fedha za makusanyo na kisha kuwataka kuendelea kukamilisha miradi ya maendeleo. Ametoa agizo hilo leo tarehe 23 juni, 2026 wakati akihutubia Mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani wa kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na Maagizo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC) 2024/25. "Siku za nyuma nilikuwa nawasema sana kwenye ukusanyaji wa mapato na matokeo duni kwenye matokeo ya elimu ya Msingi na Sekomdari ila kwa sasa mmenyanyuka sana kwenye maeneo yote hayo kwakweli napenda kuwapongeza sana na nawataka muendelee hivi hivi". RC Mtanda. Aidha, ametoa wito kwao kuendelea kusimamia matumizi mazuri ya dawa na kuhakikisha zinawafikia wananchi na kutorohusu kuzihifadhi hadi zinafikia mwisho wa matumizi jambo linaloisababishia hasara kwa Halmashauri. ...

EWURA CCC YATOA MWANGA KWA WANANCHI WASIOJUA PAKUPELEKA MALALAMIKO

Picha
  Na Hamida Ramadhan, Dodoma.  BARAZA la Ushauri la Watumiaji wa Huduma Zinazodhibitiwa na EWURA (EWURA CCC) limesema zaidi ya wananchi 500 wametembelea banda lake katika Wiki ya Utumishi wa Umma na kupata elimu, ushauri pamoja na fursa ya kuwasilisha malalamiko yanayohusu huduma za maji, umeme na gesi. Afisa Huduma kwa Wateja Mwandamizi wa EWURA CCC, Amani Mbogo, amesema baraza hilo lina jukumu la kulinda na kutetea maslahi ya watumiaji wa huduma za nishati na maji kwa kuhakikisha sauti zao zinasikika na changamoto zao zinapatiwa ufumbuzi. Akizungumza katika Wiki ya Utumishi wa Umma inayoendelea jijini Dodoma, Mbogo amesema wananchi wengi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali zinazohusiana na huduma za maji na nishati, lakini hawafahamu mahali pa kupeleka malalamiko yao ili kupata msaada. “Tumepokea wananchi wengi waliokuja kupata elimu kuhusu majukumu ya EWURA CCC, kutoa maoni, ushauri na kuwasilisha malalamiko yao. Mwitikio umekuwa mkubwa na unaonyesha umuhimu wa k...