NIMERIDHIKA NA MATUMIZI MAZURI YA FEDHA ZA HALMASHAURI - RC MTANDA




Na Mwandishi Wetu, Mwanza. 

MKUU wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewapongeza Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa kwa kufikia malengo kwenye ukusanyaji na matumizi mazuri ya fedha za makusanyo na kisha kuwataka kuendelea kukamilisha miradi ya maendeleo.

Ametoa agizo hilo leo tarehe 23 juni, 2026 wakati akihutubia Mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani wa kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na Maagizo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC) 2024/25.

"Siku za nyuma nilikuwa nawasema sana kwenye ukusanyaji wa mapato na matokeo duni kwenye matokeo ya elimu ya Msingi na Sekomdari ila kwa sasa mmenyanyuka sana kwenye maeneo yote hayo kwakweli napenda kuwapongeza sana na nawataka muendelee hivi hivi". RC Mtanda.

Aidha, ametoa wito kwao kuendelea kusimamia matumizi mazuri ya dawa na kuhakikisha zinawafikia wananchi na kutorohusu kuzihifadhi hadi zinafikia mwisho wa matumizi jambo linaloisababishia hasara kwa Halmashauri.

"Mkurugenzi wa Halmashauri hii ni mchapa kazi sana, kazi zake zinajieleza wazi ni msikivu na anajikita kwenye utendaji bora wa majukumu yake kwakweli nakupa shime endelea kufanya kazi na Waheshimiwa Madiwani mpeni ushirikiano."

Awali, Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bw. Balandya Elikana alitoa wito kwa Halmashauri hiyo kujibu hoja na mapendekezo 20 haliyobaki na kutumia fedha zilizobaki kukamilisha ukamilishaji wa miradi ya maendeleo ikiwa ni katika kuondoa kasoro na kuimarisha uwajibikaji katika ulinzi wa rasilimali za umma.

Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mkoa wa Mwanza Ndugu Richson Ringo amesema katika ukaguzi wa hesabu za mwaka 2024/25 halmashauri ya wilaya ya Buchosa imepata hati safi.








Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.