Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba 28, 2025

SALOME MNYAWI MITANO TENA KWAKE MIRERANI

Picha
  Na Mwandishi wetu, Mirerani  MGOMBEA Udiwani wa Kata ya Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Salome Nelson Mnyawi, amewaomba wakazi wa eneo hilo kumpa kura nyingi za ndiyo kwani amefanikisha maendeleo mengi katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Salome akizungumza kwenye eneo la Maduka Matatu, Mtaa wa Twiga, Kata ya Mirerani, amesema alichaguliwa kwa mara ya kwanza kipindi kilichopita hivyo anaomba kipindi kingine cha miaka mitano ili aweze kushirikiana nao kufanikisha maendeleo ya eneo hilo. Ameeleza baadhi ya mafanikio yaliyofanyika kwenye kipindi chake ni ujenzi wa kituo cha afya Tanzanite ambapo kimekamilika na sasa kinasubiria kufunguliwa na kutoa huduma kwa jamii. "Pia miundombinu ya barabara za lami kutoka soko la getini hadi lango la kuingia na kutoka ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite pamoja na taa na barabara kutoka transifoma hadi kituo cha mafuta cha Kibobo," amesema Salome. Amesema sekta ya elim...

WAPIGA KURA 273,076 WANATARAJIA KUPIGA KURA IFIKIPO OKTOBA 29, 2025 JIMBO LA IGUNGA NA MANONGA

Picha
  Na Lubango Mleka, Igunga. MSIMAMIZI wa Uchaguzi wa Majimbo ya Igunga na Manonga wilayani Igunga mkoani Tabora, Hamisi Hamisi amesema wapiga kura 273,076 wanatarajia kupiga kura ifikapo Oktoba 29, mwaka huu katika majimbo hayo. Hamisi ameeleza hayo katika ofisi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi iliyopo katika wilaya hiyo mjini Igunga. Kwa mujibu wa kifungu cha 69, (1) cha sheria ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Hamisi amewaeleza wananchi waliojiandikisha katika Daftari la Kudumu la wapiga kura la Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kuwa uchaguzi utafanyika siku ya Jumatano Oktoba 29 mwaka huu. Amesema vituo vilivyotumika kuandikisha wapiga kura katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura ndio vitatumika kupiga kura huku vikifunguliwa saa moja asubuhi na kufungwa saa 10 jioni na kwa upande wa vituo vilivyoko Magereza kufunguliwa saa mbili asubuhi na kufungwa saa tisa alaasiri. "Nitumie fursa hii kuwaomba na9999 kuwakaribisha wananchi wote wa majimbo ya Igunga na Manonga kujitokeza...