Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba 30, 2025

BALOZI WA AFRIKA KUSINI UFARANSA AKUTWA AMEFARIKI NJE YA HOTELI YA HYATT REGENCY MJINI PARISI

Picha
BALOZI wa Afrika Kusini nchini Ufaransa, Nkosinathi Emmanuel Nathi Mthethwa, amekutwa amefariki nje ya hoteli ya Hyatt Regency mjini Paris.  Ripoti zinasema alikuwa amekodi chumba ghorofa ya 22 na dirisha lilionekana limevunjika. Wizara ya Mambo ya Nje ya Afrika Kusini imethibitisha kifo chake, huku uchunguzi ukiendelea. Vyombo vya habari vya Ufaransa vimeeleza huenda alijiua.

WANAFUNZI SHULE YA MSINGI NDALA "A" WAPATIWA MAFUNZO YA NAMNA YA KUZIMA MOTO.

Picha
Konstebo Erick Costantine akiwafundisha Wanafunzi wa Shule ya Msingi Ndala "A" iliyopo Mkoani Shinyanga namna ya kuzima moto kwa kutumia fire blanket, elimu hiyo imetolewa Septemba 30, 2035 (Picha na Jeshi la Zimamoto)

RC KATAVI, WANANCHI JITOKEZENI KWA WINGI KUPATA HUDUMA ZA MATIBABU YA KIBINGWA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Katavi. WANANCHI wa Halmashauri tano (5) za mkoa wa Katavi wametakiwa kujitokeza kwa wingi ili kunufaika na huduma za matibabu ya kibingwa zinazoanza kutolewa leo na Madkatari Bingwa wa Huduma za Mkoba mkoani humo. Madaktari Bingwa wa Rais Samia wanaanza kutoa huduma leo Septemba 29, hadi Oktoba 3, 2025 mkoani katavi lengo likiwa ni kutoa tiba za kibingwa karibu na wananchi kutoka Halmashauri zote tano (5) za mkoa wa Katavi.   Mkuu wa mkoa wa Katavi Bi. Mwanavua Mrindoko ametoa wito kwa wakazi wote wenye changamoto za kiafya kujitokeza kupata huduma hiyo akisema hii ni ushuhuda mwingine wa kiutu kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.  Bi. Mrindoko amezitaja faida za uwepo wa huduma za Madaktari wa Rais Dkt. Samia kuwa ni pamoja na kutoa huduma hizo karibu kabisa na jamii, kujenga uwezo kwa watoa huduma wenyeji wa halmashauri ikiwemo kupunguza gharama za kupata huduma hizo nje ya mkoa wake. Huduma zitakazotolewa ni...