Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi 2, 2026

IRAN YASEMA HAIWEZI KUISHAMBULIA KENYA

Picha
Akizungumza jijini Nairobi, siku ya Jumatatu, Balozi wa Iran nchini Kenya Ali Gholampour, amesema kuwa makombora yatakayorushwa na nchi yake nchi yake, hayatoifikia Kenya. Gholampour anaamini kuwa, serikali ya Kenya haijatoa ngome za kijeshi kwa taifa la Marekani, zenye uwezo wa kuishambulia Iran. Hakikisho hilo linakuja wakati wa mashambulizi mfululizo katika eneo la Mashariki ya Kati, kutoka kwa Marekani na Israel, ambayo pia yalisababisha kifo cha Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, na maofisa wengine waandamizi.

WASAFIRISHAJI WA KIMATAIFA KUTUMIA AFRIKA KUSAFIRISHA MIZIGO BAHARINI

Picha
Mzozo unaoongezeka unaohusisha Marekani, Israel na Iran umevuruga mojawapo ya njia za baharini yenye shughuli nyingi zaidi duniani, na kulazimisha makampuni makubwa ya meli kuelekeza meli kuzunguka Afrika. Wasafirishaji wa kimataifa, ikiwa ni pamoja na Maersk, Hapag-Lloyd, na CMA CGM, wamesimamisha usafiri kupitia Mfereji wa Suez na Bab el-Mandeb kufuatia mashambulio ya Marekani na Israel dhidi ya Iran na kuzidisha hatari za kiusalama karibu na Mlango-bahari wa Hormuz.

WANANCHI WA MTAA CHINYOYO WACHIMBA MSINGI WA OFISI YA SERIKALI KWA NGUVU ZAO

Picha
  Na Hamida Ramadhan, Dodoma.  WANANCHI wa Mtaa wa Chinyoyo, Kata ya Kilimani, Jijini Dodoma wameanza rasmi ujenzi wa ofisi ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa kwa kuchimba msingi wa jengo hilo leo, hatua inayotajwa kuwa mwanzo wa kutatua changamoto ya muda mrefu ya kukosekana kwa ofisi rasmi ya mtaa. Kwa miaka kadhaa, wananchi wa mtaa huo walilazimika kumfuata Mwenyekiti nyumbani kwake au kwenda katika ofisi ya Mtendaji wa Kata iliyopo mtaa mwingine ili kupata huduma.  Hali hiyo imekuwa ikiwasababishia usumbufu na gharama za ziada za usafiri, hususan kwa kutumia bodaboda au bajaji. Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Chinyoyo, Mhe. Faustina Bendera, amesema kukosekana kwa ofisi kulikuwa kikwazo kikubwa katika utoaji wa huduma. “Wananchi walikuwa wanakuja nyumbani hata wakati wa shughuli binafsi. Ilibidi nisimamishe kazi za nyumbani ili kuwasikiliza na wakati mwingine kuambatana nao kufuatilia changamoto zao,” amesema. Ameongeza kuwa hata watendaji wa mtaa walikuwa wakifanya ...

WAJUMBE WA KAMATI YA JPCDS WAJIONEA MAAJABU YA HIFADHI YA NGORONGORO

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Ngorongoro.  WAJUMBE wa Kamati ya Wataalamu wa Kamisheni ya Kudumu ya Pamoja ya Ulinzi na Usalama (Joint Permanent Commission of Defense and Security – JPCDS) kutoka Tanzania na Zambia, wakiongozwa  na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Patrobas Katambi pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Jacob Jack Mwiimbu Februari 26, 2026 walipata fursa ya kutembelea na kujionea maajabu ya Hifadhi ya Ngorongoro wakati wakishiriki kikao cha siku tano Jijini Arusha kilicholenga kuimarisha ushirikiano katika kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka na matishio yanayoibukia.  Ziara hiyo ilikuwa sehemu ya kuimarisha uelewa wa pamoja kuhusu umuhimu wa kulinda rasilimali za asili kama sehemu ya ajenda ya usalama wa kikanda. Kote duniani inafahamika kuwa, Ngorongoro ni hifadhi ya kipekee duniani, iliyotokana na kaldera bonde kubwa la volkano lililosababishwa na mlipuko na kuporomoka kwa volkano kubwa takribani miaka milioni 2 hadi ...

REA YAENDELEA NA UHAMASISHAJI MIRADI YA NISHATI VIJIJINI MARA.

Picha
  Wananchi wahamasika kujiunga na huduma ya umeme.Wananchi waunga mkono matumizi ya nishati safi ya kupikia. Na Mwandishi Wetu, Mara.  WAKALA wa Nishati Vijijini (REA) unaendelea na ziara ya uhamasishaji wananchi kujiunga na huduma ya umeme pamoja na matumizi ya nishati safi ya kupikia mkoani Mara. Uhamasishaji umehusisha utoaji wa elimu kwa wananachi namna ya kufanya maombi ya kujiunga na huduma ya umeme huku lengo kuu likiwa ni  kuongeza idadi ya watumiaji wa umeme na kuwakumbusha wananchi umuhimu wa nishati ya umeme kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.  Aidha, Wakala umefanya Kampeni zinahusisha utoaji wa elimu kuhusu umuhimu na faida za matumizi ya nishati safi ya kupikia ikiwemo utunzaji wa afya, mazingira pamoja na usawa wa kijinsia.  Aidha, Wakala umetoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi bora  ya umeme hususani katika shughuli za uzalishaji ikiwemo shughuli za biashara, kilimo, na shughuli za nyumbani. Vile vile, Wakala umetoa elimu kuhusu taratibu...

REA YATOA RAI KWA WANANCHI WILAYA YA BUTIAMA KUJIUNGA NA HUDUMA YA UMEME NA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA.

Picha
Wananchi wapewa elimu ya nikonekt .Wananchi waaswa kutumia nishati safi na salama ya kupikia. Na Mwandishi Wetu, Butiama. WAKAZI wa wilaya ya Butiama Mkoa wa Mara,waaswa kutumia nishati safi na salama ya kupikia, kujiunga na huduma ya umeme  pamoja na  kutunza miundombinu ya umeme ili miundombinu hiyo iweze kudumu na  kutoa huduma kwa wananchi kwa  mda mrefu. Rai hiyo imetolewa leo jumatatu Machi 02, 2026 na wataalamu wa REA na TANESCO walipofika katika wilaya hiyo kutoa elimu na uhamasishaji wa miradi ya nishati vijijini. Akizungumza wakati wa uhamasishaji Afisa maendeleo ya jamii kutoka REA , ndugu Abdulrazack Mkomi amesema, Kwa sasa taratibu za uombaji huduma ya umeme zimeboreshwa zaidi  na hakuna tena mambo ya kutumia fomu kufanya maombi ambapo kwa kutumia tu namba ya Nida mwananchi anaweza kufanya ombi la  umeme moja kwa moja TANESCO kupitia huduma ya NIKONEKT. “Kwa kutumia simu janja, mwananchi atapakua huduma ya Nikonekt na kufanya maombi au kama ni ...