IRAN YASEMA HAIWEZI KUISHAMBULIA KENYA




Akizungumza jijini Nairobi, siku ya Jumatatu, Balozi wa Iran nchini Kenya Ali Gholampour, amesema kuwa makombora yatakayorushwa na nchi yake nchi yake, hayatoifikia Kenya.

Gholampour anaamini kuwa, serikali ya Kenya haijatoa ngome za kijeshi kwa taifa la Marekani, zenye uwezo wa kuishambulia Iran.

Hakikisho hilo linakuja wakati wa mashambulizi mfululizo katika eneo la Mashariki ya Kati, kutoka kwa Marekani na Israel, ambayo pia yalisababisha kifo cha Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, na maofisa wengine waandamizi.







Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.