Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba 25, 2025

POLISI WAANZA UCHUNGUZI KUHUSU KUTEKWA KWA POLEPOLE, WAKISISITIZA KUMUHITAJI KWA DCI

Picha
Na Hamida Ramadhani, Dodoma. JESHI la Polisi nchini Tanzania, kupitia kwa Msemaji wake DCP David Misime, limesisitiza kuwa bado linaendelea kumsubiri Ndugu Humphrey Polepole ili aripoti katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), kwa ajili ya kutoa maelezo kuhusu tuhuma mbalimbali alizozitoa kupitia mitandao yake ya kijamii. Ikumbukwe kuwa mnamo Jumatatu, Septemba 15, 2025, Jeshi la Polisi lilitangaza kuwa limefungua jalada la uchunguzi na linaendelea kuchunguza tuhuma hizo ambazo kada huyo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amekuwa akizitoa.  "Tuhuma ambazo ametoa na anaendelea kuzitoa, kulingana na jinsi alivyozielezea, zinaashiria uwepo wa makosa ya jinai kwa mujibu wa sheria, makosa haya yanahitaji ushahidi wa kuzithibitisha zitakapowasilishwa mahakamani. Tuhuma hizo amekuwa akizitoa kupitia mitandao ya kijamii. Baada ya kufungua jalada na kuanza uchunguzi, Jeshi la Polisi, mbali na kukusanya ushahidi, limekuwa likifanya jitihada za kumpata ili aweze kutoa mael...