Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei 21, 2026

NCHIMBI AAGIZA VIONGOZI WANAOWAKWAMISHA WAANDISHI WAENDESHA OFISI KUCHUKULIWA HATUA

Picha
  Na Happyness Hans, WAF - ARUSHA  MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe.Dkt. Emmanuel Nchimbi amewataka viongozi na wakuu wa Idara wanaowazuia waandishi waendesha Ofisi kushiriki mikutano ya chama hicho kuchukuliwa hatua za kinidhamu. Amesema hayo leo Mei 21, 2026 Mkoani Arusha kwa niaba ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan wakati akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa 13 wa Waandishi Waendesha Ofisi Tanzania (TAPSEA), unaoambatana na uchaguzi wa viongozi wapya wa chama hicho. “Tunatamani kila kiongozi awapende, awajali, awape safari, motisha na kuwapongeza pale wanapofanya vizuri,” amesema Dkt. Nchimbi. Mhe. Dkt. Nchimbi amesema Ofisi yoyote bila uwepo wa waandishi waendesha Ofisi ni sawa na gari lisilo na usukani, kwani wao ndiyo sura na lango la Ofisi. Amesema hakuna mtu anayeweza kuonana moja kwa moja na kiongozi bila kupitia kwa mwendesha Ofisi. Aidha amesema waandishi waendesha Ofisi wamekuwa msaada mkubwa katika Taasisi mbalim...

AFROMEDIA YAIPONGEZA "CAIRO 24" KWA KWA KUTWAA TUZO YA "TOVUTI BORA ZAIDI MASHARIKI YA KATI"

Picha
Na Mwandishi Wetu, Cairo.  HASSAN Ghazaly, Mwanzilishi wa Mpango wa “Afromedia kwa Uandishi wa Habari na Vyombo vya Habari vya Afrika”, ametoa pongezi zake za dhati kwa wahariri wa tovuti ya “Cairo 24”, wakiongozwa na mwanahabari Mahmoud El-Mamlouk, Mhariri Mkuu, kwa mnasaba wa kutunukiwa kwa tovuti hiyo na kutwaa tuzo ya “Bora zaidi Mashariki ya Kati” katika hafla ya utoaji wa tuzo za Trend Awards.  Mafanikio haya yanaakisi nafasi madhubuti ya kitaaluma na kimedia ambayo tovuti hiyo imefanikiwa kuijenga katika kipindi kifupi nchini Misri na barani Afrika. Ghazaly alieleza kuwa kutunukiwa kwa “Cairo 24” kunawakilisha mfano wa vyombo vya habari wenye ushawishi mkubwa katika medani ya habari barani Afrika na nchini Misri, ulioweza kuunganisha kasi, usahihi na uaminifu katika uwasilishaji wa habari, pamoja na mchango wake katika kufuatilia masuala ya kikanda na kimataifa, hasa yale yanayohusiana na bara la Afrika na mataifa yake. Aidha, Hassan Ghazaly alisifu mafanikio hayo, akib...