Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari 27, 2026

WADAAWA WA KIIRAQW WAPATA NAFASI YA KUSIKILIZWA KWA LUGHA YAO, BARAZA LA ARDHI DODOMA LATOA TUMAINI LA HAKI SAWA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  BARAZA la Ardhi na Nyumba la Wilaya, Mkoa wa Dodoma limewasikiliza wananchi wa jamii ya Kiiraqw waliofika katika Baraza hilo kuwasilisha hoja na ushahidi wao katika mgogoro wa ardhi, wakidai kumiliki kihalali shamba lenye ukubwa wa ekari nane lililopo Wilaya ya Chamwino, Mkoa wa Dodoma. Hatua hiyo imekuja kufuatia maombi ya wadaawa hao ambao ni pande mbili zinazohusika katika shauri hilo, kubainisha kuwa wanakabiliwa na changamoto ya lugha, hali iliyokuwa ikiathiri uwezo wao wa kujitetea na kueleza kwa uwazi hoja zao mbele ya Mwenyekiti wa Baraza hilo, Mhe. Omary Mbega. Kutokana na hilo, Baraza lilitoa huduma ya ukalimani kupitia mkalimani, Ndg. Simon Tlatlaa Emmay, ambaye alitafsiri maelezo yao na kuwawezesha wadaawa hao kufafanua kwa kina madai yao, kuwasilisha ushahidi pamoja na vielelezo muhimu bila kikwazo cha lugha. Shauri hilo ni Shauri la Ardhi Na. 92 la mwaka 2025, linalomhusu Ekaristi Ngu’nda kama Mleta Maombi dhidi ya Lolote Nanacha na ...

VIJANA MWANZA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZINAZOTOLEWA NA HALMASHAURI.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Mwanza.  RAI hiyo imetolewa leo Februari 27, 2026 na Mkuu wa Wilaya ya Magu,Jubilate Lawuo wakati akifungua maadhimisho,Elimu na uzinduzi wa mitambo katika teknolojia ya ukandarasi wa madini ambapo madhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya Nyamhongolo jijini mwanza.  Lawuo amesema mikopo ya Halmashauri inasaidia sana vijana katika kujiajiri kwa mtu mmoja , mmoja au vikundi. " Serikali yetu imeweka mazingira mazuri kwa vijana wetu kukopeshwa kupitia vikundi vyao. Pia na Halmashauri zetu zinajitaid sana katika kusaidia vijana wetu" alisema. Vile vile, Lawuo ameagiza  vijana waweze kujitokeza kwa wingi katika maonyesho ya wakandarasi ili waweze kuona mitambo mbalimbali ya uchimbaji na ukandarasi inayopatikana. Ameongeza kuwa mkoa wa Mwanza katika wilaya za Kwimba na Sengerema kuna migodi mbalimbali iliyoajiri vijana wa kitanzania wanaojihusisha na uchimbaji wa madini. Naye Mwenyekiti wa maonyesho ya wakandarasi na wachimbaji, George Mandia alisema mao...

TUITUNZE AMANI KWA UHAKIKA WA KUPATA HAKI MSINGI NA MAHITAJI MUHIMU- BI. MBEGU

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam.  WAKAZI wa Dar Es Salaam wameeleza umuhimu wa amani nchini, Watanzania wakitakiwa kujifunza kutoka kwa mataifa yasiyokuwa na amani namna ambavyo wamekuwa wakipitia changamoto kubwa za kiuchumi na kijamii. Akizungumza na waandishi wa habari, Bi Amina Mbegu Rashid, Mkazi wa Dar Es salaam, ameeleza amani ndio msingi wa uhuru wa wananchi kufanya shughuli zao, akisema amani pia imesababisha Taifa kupiga hatua kubwa za maendeleo ambapo bila amani huenda Taifa lisingeshuhudia maendeleo na ustawi uliopo sasa katika nyanja mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa haki za binadamu. "Amani kwenye Taifa letu ni muhimu sana, imetupa nafasi na uhuru wa kufanya mambo yetu bila shuruti. Kwenye nchi za wenzetu kuna shida nyingi sana ambapo hata kutembea tu imekuwa changamoto, hapa kwetu hakuna mwenye viroba 20 ama 30 ndani vya chakula kwahiyo amani ikitoweka unaweza kuona changamoto ambayo tutaipitia hasa katika upatikanaji wa huduma muhimu ikiwemo za matibabu kwah...

AMANI YATAJWA KAMA FURSA MUHIMU YA WANANCHI KUJIENDELEZA KIUCHUMI

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam.  BWANA Rashid Kengwa Rashid Mkazi wa Ilala Mkoani Dar Es Salaam amesema kukosekana kwa amani katika jamii kunakwamisha maendeleo na ustawi wa wananchi pamoja na kutatiza uhuru wa wananchi kufanya shughuli zao za kijamii na kiuchumi, msisitizo akiutoa kwa kila mwananchi kuwajibika kuilinda na kukataa vitendo vyenye kuhatarisha amani na usalama wa Tanzania. "Suala la amani ni jambo la kushukuru kwasababu lipo kwa kiasi kikubwa sana na pasingekuwa na amani hata hapa nisingezungumza nanyi, tungekuwa ni watu wa kujificha tu na tumshukuru Mungu sana kwa amani hii aliyoendelea kutupatia." Amesema Bw. Rashid. Rashid ameeleza pia tofauti ya Tanzania na mataifa mengine yasiyokuwa na utulivu na amani, akisema kukosekana kwa amani kumesababisha madhila makubwa kwa watu wengi ikiwemo vifo, kuongezeka kwa umaskini pamoja na kukosekana kwa uhuru na hivyo kuua fursa za raia kujiendeleza kiuchumi pamoja na kuishi katika wasiwasi na hofu.