Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti 2, 2025

GST YATOA USHAURI NA UPIMAJI SAMPULI ZA MAJI, MIAMBA NA MADINI.

Picha
Wizara ya Madini yaendelea kutoa elimu ya Sheria, Kanuni za Madini.  Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  TAASISI ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imeendelea kutoa ushauri na huduma za upimaji wa sampuli za miamba na madini kwa wananchi mbalimbali wanaofika kutaka kujua aina za miamba na madini waliokuwanayo. Aidha, GST imekuja na vifaa vya utafiti wa miamba na madini iliyo chini ya tabaka ya juu la udongo ambavyo kitaalam vinaitwa vifaa vya jiofizikia. Sambamba na hayo, Wataalamu kutoka GST wamewashauri wananchi kutumia Maabara ya taasisi hiyo kwa uchunguzi wa sampuli zao za miamba na madini ili kubaini wingi na uwepo wa madini ili kuongeza tija na uzalishaji wa madini. Aidha, Wizara ya Madini kwa kushirikiana na taasisi zake imeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya sekta ya madini kupitia banda lake lililopo katika eneo la mabanda ya Serikali, banda namba 5. Kupitia banda hilo, wananchi wanaelimishwa kuhusu shughuli mbalimbali zinazohusu sekt...

KATIBU MKUU MIFUGO, UVUVI AHIMIZA UTOAJI ELIMU KWA UMMA KUHUSU SHUGHULI ZA OFISI YA WAZIRI MKUU.

Picha
Na Mwandishi Wetu, DODOMA.  KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Agnes Meena ametoa rai kwa Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu waendelee kutoa elimu kwa wananchi kuhusu utendaji wa taasisi na programu mbalimbali zinazosimamiwa na Ofisi hiyo. Kauli hiyo ameitoa leo tarehe 02 Agosti, 2025 alipotembelea banda la Ofisi hiyo akiwa ameambatanan na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Dkt. Stephen Nindi na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri katika Maonesho ya Naneane yanayofanyika Viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma. “Wananchi wanauhitaji Mkubwa wa kufahamu shughuli zinazoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, hivyo kuna umuhimu wa kuandaa vipindi vya kuelimisha umma,” ameeleza. Maonesho ya Wakulima maarufu Nanenane yamebebwa na kauli mbiu isemayo: "Chagua Viongozi Bora, kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025"

KARIBU BANDA LA HALMASHURI YA IGUNGA KWENYE MAONESHO YA NANE NANE MKOANI TABORA.

Picha
 

COOP BANK YAJIVUNIA UTOAJI HUDUMA SEKTA YA KILIMO.

Picha
. Coop Bank yatangaza Ushiriki Mkubwa katika Maonesho ya Nanenane, Na Mwandishi Wetu, Dodoma.  BENKI ya Ushirika Tanzania (Coop Bank) imethibitisha kushiriki kikamilifu katika Maonesho ya Kitaifa na Kimataifa ya Nanenane 2025 yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma, ikiwa ni miongoni mwa wa  dhamini wa maonesho hayo makubwa ya kilimo nchini. Akizungumza na waandishi wa habari katika banda la benki hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Coop Bank, Bw. Godfrey Ng’urah, amesema benki hiyo imejikita katika kutoa huduma za kifedha zenye kuleta mabadiliko chanya katika mnyororo mzima wa thamani wa kilimo-biashara, huku ikitoa kipaumbele kwa wakulima, vijana na wajasiriamali wa vijijini. “Coop Bank ni benki ya ushirika kwa vitendo. Zaidi ya asilimia 51 ya umiliki wake upo mikononi mwa vyama vya ushirika hii ni benki ya wakulima, kwa wakulima,” amesema Bw. Ng’urah. Ameeleza kuwa, Benki hiyo inashirikiana na vyama vya msingi (AMCOS) na vyama vikuu vya ushirika (UNION) nchini kote...