Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai 26, 2025

HAKI ZA MWANDISHI WA HABARI WAKATI WA UCHAGUZI.

Picha
 

KAMATI YA UKAGUZI TARURA YATEMBELEA MIRADU MINNE YA BARABARA SHINYANGA.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Shinyanga.  IKIWA katika muendelezo wa ziara yake ya kutembelea utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa miundombinu ya barabara, Kamati ya Ukaguzi ya TARURA  imetembelea Miradi minne ya ujenzi wa miundombinu ya barabara mkoani Shinyanga.  Katika Manispaa ya Shinyanga Kamati ilitembelea ujenzi wa barabara ya Old Shinyanga-Chibe-Negezi kiwango cha changarawe  na ujenzi wa Kalavati na daraja la Mawe la Nin'ghwa katika barabara hiyo.  Vile vile kamati hiyo ilipata fursa ya kutembelea mradi wa ujenzi wa barabara ya Kinyata-Karena yenye urefu wa Km 0.8 kwa kiwango cha lami inayojengwa Kata ya Kambarage katika Manispaa hiyo.  Pia, Kamati imetembelea Mradi wa uondoaji vikwazo wa ujenzi wa Daraja la seli sita linalojengwa katika barabara ya Magonzo-Shinyanga unaotekelezwa chini Mradi wa  RISE pamoja na mradi wa ujenzi wa barabara ya DED-DC Km 1.0 kwa kiwango cha lami Wilayani Kishapu.  Akielezea manufaa ya Miradi hiyo kiuchumi na kijamii, Men...

MGAWANYO WA MINARA YA MAWASILIANO YA SIMU.

Picha
HADI kufikia Juni 2025, idadi ya minara ya huduma ya mawasiliano ya simu ilikuwa ni 9,448. Mkoa wa Dar es Salaam unaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya minara 1,222. Mikoa mingine ni Morogoro yenye minara 501, Dodoma minara 479, Mwanza yenye minara 453, na Tanga minara 434. Mgawanyo wa idadi ya minara kwa kila mkoa imeoneshwa kwenye ramani 1.6. Tembelea tovuti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) (www.tcra.go.tz), au kupitia kiunganisho https://bit.ly/44tXbii ilikupitia ripoti kamili ya takwimu ya sekta ya Mawasiliano (Aprili - Juni 2025).  

TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA HUDUMA YA UMEME MKOA WA ARUSHA

Picha
 

MBOSO ATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA ILEMELA.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Ilemela - Mwanza.  MSANI wa kizazi kipya Mbwana Yusuph Kilungi (Mbosso) amefika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe Amir Mkalipa kwa ajili ya kujitambulisha na pia kufanya tendo la hisani kwa kutoa msaada kwa kituo cha Hisani ambacho kinahudumia watoto yatima na wenye mahitaji maalum kilichopo wilayani hapa Mhe Mkalipa akimkaribisha msanii huyo, alitumia wasaa huo kumueleza fursa mbalimbali zilizopo wilayani hapa lakini pia kumshauri juu ya kuwekeza kwani wakati ni sasa. Mbisso akiwa katika kituo cha hisani ameweza kula chakula cha mchana na watoto hao na ametoa misaada mbalimbali ikiwemo magodoro, chakula, vyandarua n.k, lakini pia ameahidi kuchangia bima ya afya ya watoto hao.

DKT.MWINYI ASHIRIKI MKUTANO MKUU MAALUM WA CCM TAIFA

Picha
   MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar , Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameshiriki Mkutano Mkuu Maalum wa CCM ulioongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa njia ya kidijitali ambapo ameongea na Wajumbe wa Mkutano huo Nchi nzima kwa njia ya Mtandao leo tarehe 26, Julai 2025 katika ukumbi wa Mkutano wa NEC(White House) Makao Makuu ya CCM Jijini Dodoma.

RC PAUL CHACHA KUHAMASISHA WANANCHI KUJITOKEZA KATIKA UCHAGUZI MKUU OCTOBA, 2025.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Uyui - Tabora.  MKUU wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha amemuahidi Mkimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2025, Ismail Ussi kuendelea kuwahamasisha wananchi washiriki uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na  Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu. Chacha ametoa wito huo wakati wa mapokezi na makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru 2025 yaliofanyika katika viwanja vya shule ya sekondari Tura wilayani Uyui mkoani hapa. Amedokeza Mwenge wa Uhuru unatembelea, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo 57 yenye thamani ya sh. 38.8 bilioni. Kwa upande wa Mkimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2025, Ismail Ussi aliahidi kulinda heshima ya wananchi wa mkoa huo huku akiwashukuru na kuwapongeza wananchi kwa kujitokeza kwa wingi katika mapokezi na makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru.

MRADI WA SEQUIP KUMKOMBOA MTOTO WA KIKE DAR ES SALAAM NA RUVUMA.

Picha
Na Mwandishi Wetu.  SERIKALI inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia Mradi wa kuboresha elimu ya sekondari-SEQUIP imekamilisha ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika shule mpya za Sekondari za wasichana Dar es salaam na Ruvuma. Pamoja na dhamira hiyo ya serikali ya kuboresha sekta ya elimu kwa kuwekeza na kufanya ujenzi na ukarabati wa miundombinu kwenye shule na vyuo, pia ikiwajengea Walimu uwezo wa kiutendaji kupitia mafunzo yanayoendelea kutolewa kupitia mradi wa kuimarisha Shule Salama za Sekondari (SEQUIP). Katika kutimiza azma ya kuboresha sekta ya elimu nchini, Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia inatekeleza mradi huo wa SEQUIP kwa thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 500 ambazo ni sawa na shilingi Bilioni 1.2 kwa kipindi cha miaka mitano. Tangu kuanza kwa mradi huo mwaka wa fedha wa 2021/2022, Serikali imejenga shule mpya za sekondari na kufanya ukarabati mkubwa wa miundombinu pamoja na kutoa mafunzo ya kujenga u...