MGAWANYO WA MINARA YA MAWASILIANO YA SIMU.
HADI kufikia Juni 2025, idadi ya minara ya huduma ya mawasiliano ya simu ilikuwa ni 9,448. Mkoa wa Dar es Salaam unaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya minara 1,222.
Mikoa mingine ni Morogoro yenye minara 501, Dodoma minara 479, Mwanza yenye minara 453, na Tanga minara 434. Mgawanyo wa idadi ya minara kwa kila mkoa imeoneshwa kwenye ramani 1.6.
Tembelea tovuti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) (www.tcra.go.tz), au kupitia kiunganisho https://bit.ly/44tXbii ilikupitia ripoti kamili ya takwimu ya sekta ya Mawasiliano (Aprili - Juni 2025).

Maoni