Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti 9, 2025

UJENZI WA JENGO LA UBIA KATI YA NHC NA TOSH LOGISTICS KARIAKOO.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Kariakoo- Dar es Salaam.  SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) kwa ubia na Tosh Logistics Ltd linaendelea na ujenzi wa jengo la kisasa la biashara na makazi katika eneo la Tandamti, Kariakoo – Dar es Salaam. Mradi huu unaojengwa kwenye viwanja sita (3/16 hadi 14/16) unalenga kubadilisha sura ya Kariakoo kwa kujenga majengo ya kisasa yenye matumizi mchanganyiko. Jengo limegawanywa katika Block A na Block B ambapo kazi zinasonga mbele kwa kasi, block A ipo hatua ya ujenzi wa ghorofa ya pili, block B imefikia ghorofa ya sita. Mradi huu unatekelezwa kuanzia Oktoba 15, 2024 hadi Oktoba 15, 2026, ni sehemu ya jitihada za NHC kukuza miundombinu ya kisasa na kuchochea uwekezaji kwenye maeneo ya mijini kupitia ubia wa kimkakati na sekta binafsi. #NHCProjects #ToshLogistics #MajengoYaKisasa #KariakooMpya #UjenziEndelelevu #PublicPrivatePartnership #MaishaNiNyumba#CrownMedia #Ayotv

MATUKIO KATIKA PICHA.

Picha
MGOMBE wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya ACT Wazalendo Ndugu Luhaga Mpina, Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Fatma Ferej na Mgombea wa Urais wa Zanzibar Ndugu Othman Masoud Othman wamepokelewa na maelfu ya wanachama wa ACT Wazalendo na wananchi wa Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha upande wa Unguja leo tarehe 9 Agosti 2025. Oktoba #LindaKura #MuhuniHasusiwi @ACTwazalendo

RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS.

Picha
Dodoma. RAIS DKT. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 09.08.2025  akiwa na Mgombea Mwenza DKT. Balozi Emmanuel Nchimbi wamefika katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais na Makamu wa Rais kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu Octoba 2025.

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Tabora.  HALMASHAURI ya Wilaya ya Igunga imeibuka mshindi wa kwanza katika kundi la Mamlaka za Serikali za Mitaa (Tabora na Kigoma) wakati wa Maonesho ya Nanenane mwaka 2025 ngazi ya kanda yaliyofanyika Uwanja wa Maonesho Ipuli - Tabora. Aidha, imeshika nafasi ya pili katika kundi la washindi wa jumla wa mikoa ya Tabora na Kigoma wakati wa Maonesho hayo. Akizungumza baada ya Halfa hiyo, Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Ndug. Elizabeth Rwegasira amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Selwa Hamid kwa ushirikiano mzuri na Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Grace Nyamwanji kwa kufanikisha ushindi huo. Kwa upande wa Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Halamshauri hiyo, Grace Nyamwanji amewashukuru na kuwapongeza, Wakuu wa Idara na Vitengo, Watumishi na  Wadau wote waliyoshiriki maonesho hayo kwa sababu wao ndio chachu ya ushindi huo.