WANANCHI WA KATEMBE, MWALONI MULEBA WAONDOKANA NA ADHA YA BARABARA
*Ni kiunganishi cha wafanyabiashara wa Rwanda, Burundi na Uganda* Na Mwandishi Wetu, Muleba. UJENZI wa barabara ya lami ya Katembe -Mwaloni inayounganisha Barabara kuu ya kutoka nchi za Uganda, Rwanda na Burundi katika wilaya ya Muleba Mkoani Kagera uliogharimu zaidi ya shilingi Milioni 400 umeleta ahueni kwa wakazi wa eneo hilo pamoja na wafanyabiashara wa samaki kutoka katika visiwa vilivyopo ndani ya ziwa Victoria kwenda ndani na nje ya Nchi. Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Ndugu Ismail Ussi ameridhisha na viwango vya mradi huo na kuwapongeza TARURA kwa utekelezaji wa mradi wenye viwango ambao unaendeleaa kuwasaidia wananchi . Alisema kuwa Ili wanachi wapate huduma bora na nguvu ya kuzalisha wanahitaji Barabara nzuri zenye viwango na kupitia umma wa wananchi ameshukuru usimamizi wa mradi huo na namna Halmashauri ya Muleba ulivyotoa mapato ya ndani kujenga Barabara imara inayoweza kuchochea uchumi na kuvutia wawekezaji na wafanyabiashara...