TRA YAKARIBISHWA MAKANISANI KUTOA ELIMU YA KODI
Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro.
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Kilimanjaro imealikwa kutoa elimu ya kodi kwa Wanachama wa ELCT SACCOS katika kikao cha mwaka cha taasisi hiyo.
Mafunzo hayo yamefanyika jana tarehe 06.09.2025 katika Kanisa la KKKT ushirika wa Majengo , katika manispaa ya Moshi, Mwika na Hai mkoani Kilimanjaro ambapo mada zilizowasilishwa ni pamoja na Usajili wa biashara mtandaoni, Dawati maalumu la uwezeshaji biashara na uwasilishaji wa ritani za kodi na ulipaji wa kodi kwa hiari.
Akiwasilisha mada, Afisa Msimamizi wa Kodi Mwandamizi, Bw. Odupoi Papaa amewasisitiza wanachama kuwasilisha ritani za kodi na kufanya ya kodi kwa wakati pamoja na kutoa na kudai risiti za kielektroniki.





Maoni