MRADI WA ESP KUNUFAISHA WASICHANA ZAIDI YA 60 NZEGA.
Na Allan Kitwe, Tabora. WASICHANA zaidi ya 60 wanaotoka katika familia zisizo na uwezo Wilayani Nzega Mkoani Tabora wanatarajiwa kunufaika na mradi wa uwezeshaji mtoto wa kike kupata ujuzi (Empowerment Through Skills Program in Tanzania-ESP). Mradi huo unaofadhiliwa na nchi ya Canada (Canada Fund) kwa lengo la kuwezesha watoto wa kike wanaoishi katika mazingira magumu kupata fursa za ujuzi, unatekelezwa katika Vyuo 12 viivyopo katika Mikoa zaidi ya 8 hapa nchini. Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Mwanhala, Nzega ni miongoni mwa vyuo 12 vilivyoingizwa katika program ya ufadhili ili kutoa mafunzo hayo ya muda mfupi (short course) kwa watoto wa kike. Akizungumza juzi na waandishi wa habari kwa niaba ya Mkuu wa Chuo hicho Enock Lalida, Afisa Utumishi Hekima Amri Lupembe ameeleza kuwa mradi huo ni muhimu sana kwa kuwa unawapa fursa watoto wa kike kupata ujuzi. ‘Wasichana 30 wanaotoka katika kaya zinazoishi katika mazingira magumu Wilayani hapa tayari wamesajiliwa na kuan...