Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba 4, 2025

DKT. HUSSEIN ALI MWINYI AZINDUA SOKO LA KISASA CHUINI ZANZIBAR

Picha
  RAIS wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amezindua soko la kisasa la wafanyabiashara Chuini, lililopo Wilaya ya Magharibi A. Soko hilo limejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 43 na lina uwezo wa kutoa ajira kwa wananchi 4000 na kuchangia ukuaji wa uchumi wa eneo hilo. Akizungumza wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa soko hilo, Rais Mwinyi amesema malengo makuu ya serikali ni kuhakikisha wafanyabiashara wanapata mazingira mazuri ya kufanya biashara, huku wakichangia maendeleo ya kiuchumi na kutengeneza fursa za ajira kwa jamii.  Ameahidi kuwa serikali itaendelea kuwekeza katika miradi inayoongeza tija na ustawi wa wananchi.

MRADI WA MAJIKO BANIFU WATAMBULISHWA KIGOMA

Picha
*Majiko banifu 8,424 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku mkoani Kigoma *Wilaya Sita kunufaika na mradi.  *Kila Wilaya kupata majiko 1,404.  Na Mwandishi Wetu, Kigoma.  WAKAZI wa Kigoma waaswa kuunga mkono jitihada za Serikali katika utunzaji wa mazingira kwa kutumia nishati safi na salama ya kupikia Wito huo umetolewa leo Septemba 04, 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Simon Nyakoro Sirro wakati akipokea mradi wa uuzaji na usambazaji wa majiko banifu unaosimamiwa na kuratibiwa  na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) . "Kinachofanyika leo ni kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za matumizi ya nishati safi na salama katika kutunza mazingira na kuboresha Afya za wananchi" amesema Mkuu wa mkoa Mhe. Sirro, alipokuwa akipokea mradi huo. Akiwasilisha taarifa ya mradi kwa mkuu wa mkoa, Mhandisi wa Miradi kutoka wakala wa Nishati Vijijini (REA), Raya Majallah amesema, “Mradi huu unalenga kusambaza majiko banifu ili kukuza upatikanaji wa Nishati safi na...

MRADI WA TACTIC KUPUNGUZA MSONGAMANO WA MAGARI JIJINI MWANZA

Picha
Sekta ya uvuvi nayo yaguswa.  Na Mwandishi Wetu, Mwanza.  UJENZI wa Barabara ya Buhongwa-Igoma yenye urefu wa Km 14 kwa kiwango cha lami inayojengwa katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza inatajwa kuwa ndio mwarobaini wa changamoto ya msongamano wa magari jijini humo.  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Wakili Kiomoni Kibamba wakati akielezea hali ya utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Jiji la Mwanza kupitia Mradi wa Uendelezaji Miji na Majiji Tanzania (TACTIC)  na manufaa yake kwa wananchi. Amesema barabara hiyo inayounganisha Kata nne ambazo ni Buhongwa, Lwanhima, Kishiri na Igoma ilikuwa na changamoto kubwa hali iliyopelekea magari yote yaliyokuwa yakitoka Buhongwa kwenda Igoma au Igoma kwenda Buhongwa kulazimika kuingia katikati ya jiji hivyo kuongeza msongamano wa magari.  Wakili Kibamba ameongeza kuwa  ujenzi wa barabara hiyo utasaidia kupunguza msongamano huo kwa kiasi kikubwa kwani magari yote yaliyokuwa yanatoka maeneo ...

HELKOPTA YAPOTEA NA WATU NANE

Picha
HELKOPTA yenye watu wanane imepotea kwenye kisiwa cha Borneo, Indonesia, na juhudi za uokoaji zimeanza, kwa mujibu wa maafisa wa uokoaji. Kiongozi wa shirika la uokoaji Banjarmasin, I Putu Sudayana, amesema helikopta hiyo ilikuwa na marubani wawili na abiria sita, na wanatarajia kuwapata wote wakiwa salama ndani ya siku saba za utafutaji. #indonesia #borneo #banjarmasin #indonesiahelicopter

CCM YAJIVUNIA MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO, YA AHAIDI KUBORESHA ELIMU, MAJI NA VIPAJI VYA VIJANA

Picha
  Na Hamida Ramadhan, Dodoma CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimesema mafanikio ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati nchini ni kielelezo cha dhamira yake ya kweli katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli, na kwamba kinaendelea kujipanga kuimarisha huduma muhimu za kijamii katika kila sekta. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM katika Jiji la Dodoma, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtumba, Anthony Mavunde, amesema pamoja na mafanikio ya miradi kama ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), usambazaji wa umeme vijijini kupitia REA, na barabara kuu za lami, CCM ina mpango kabambe wa kuwekeza zaidi katika elimu, maji, miundombinu ya afya na kukuza vipaji vya vijana. “Huduma bora kwa wananchi ndiyo msingi wa maendeleo ya kweli. Tutaendelea kupeleka umeme kwenye vijiji vilivyobaki, kuboresha miundombinu ya shule na zahanati, na kuhakikisha kila kijiji kinapata maji safi na salama,” amesema Mavunde. Ameeleza kuwa serikali kupitia CCM inaendelea kutekeleza programu maalum za kuibua na ...