Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba 24, 2025

MULIRO AONYA WANAOPANGA KUANDAMANA NA KUFANYA VURUGU DSM Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amewaonya wale wote wanaopanga, kuratibu ama kutaka kushiriki kwenye uvunjifu wa amani ikiwemo kufanya vurugu na maandamano Oktoba 29, 2025, akisema Jeshi hilo limekula kiapo kulinda nchi pamoja na raia na mali zao. Kamanda Muliro ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Oktoba 24, 2025 wakati wa kongamano la Vyuo na Vyuo Vikuu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Kongamano lililofanyika kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza na kuwashirikisha wanafunzi wa shule za Sekondari, Vyuo na Vyuo Vikuu, akiwataka Vijana pia kuwa waangalifu na kutafakari kuhusu misukumo na mihemko yao kulingana na aina na makundi ama watu wanaoambatana nao. "Tukiwa kama watu tuliokula kiapo tunawaleza kuwa tutatimiza jukumu letu la kuhakikisha kuwa watu wanakuwa salama, watu wajitokeze kwa wingi kupiga kura, wafuate sheria na sisi tutakuwepo barabara kuwalinda wote wanaoenda kutimiza jukumu lao la Kikatiba la kwenda kupigakura. Siku hiyo kutakuwa hakuna maandamano wala hakuna vurugu, siku hiyo ni ya upigaji wa kura bila hofu."Amesema. Kama Muliro pia amesisitiza kuwa Vijana kuwa na fikra chanya ama hasi katika kujadili jambo fulani sio kitu kibaya ila kuipeleka mitazamo hasi kwenye vitendo vya vurugu ndiyo kosa kisheria, akiwataka pia Vijana kulinda hatma zao kwa kuhakikisha nchi inakuwa na amani ili kuwawezesha kutimiza malengo na ndoto zao kiuchumi, kisiasa na Kijamii.

Picha
Na Lubango Mleka, Dar es Salaam. KAMANDA wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amewaonya wale wote wanaopanga, kuratibu ama kutaka kushiriki kwenye uvunjifu wa amani ikiwemo kufanya vurugu na maandamano Oktoba 29, 2025, akisema Jeshi hilo limekula kiapo kulinda nchi pamoja na raia na mali zao. Kamanda Muliro ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Oktoba 24, 2025 wakati wa kongamano la Vyuo na Vyuo Vikuu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Kongamano lililofanyika kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza na kuwashirikisha wanafunzi wa shule za Sekondari, Vyuo na Vyuo Vikuu, akiwataka Vijana pia kuwa waangalifu na kutafakari kuhusu misukumo na mihemko yao kulingana na aina na makundi ama watu wanaoambatana nao. "Tukiwa kama watu tuliokula kiapo tunawaleza kuwa tutatimiza jukumu letu la kuhakikisha kuwa watu wanakuwa salama, watu wajitokeze kwa wingi kupiga kura, wafuate sheria na sisi tutakuwepo barabara kuwalinda wote wanaoenda kutimiza jukumu lao la Kikatiba la kwenda ...

VIONGOZI WA DINI WAKEMEA WANAOTAKA KUANDAMANA

Picha
Na Allan Kitwe, Tabora. VIONGOZI wa madhehebu ya dini kutoka Mikoa ya Tabora, Kigoma na Katavi wameiasa jamii kutojihusisha na vitendo vya uvunjifu amani ikiwemo kushiriki maandamano yanayolenga kuvuruga amani na utulivu wa nchi. Wakiongea katika Kongamano Maalumu la Amani lililofanyika leo katika ukumbi wa Panasonic Mjini Tabora wameeleza kuwa maandamano na vurugu hayajengi bali yanabomoa misingi ya amani na kuongeza chuki na uhasama. Akifungua Kongamano hilo Shehe wa Mkoa wa Tabora Ibrahimu Mavumbi ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Maridhiano ya Amani ya Mkoa amesema kuwa amani ni tunu muhimu sana kwa maendeleo ya taifa lolote lile. Amesisistiza kuwa ni muhimu sana jamii ikaelimishwa umuhimu wa kudumisha amani na upendo na kujiepusha na vitendo vyovyote vinavyoashiria uvunjifu wa amani katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu Oktoba 29. ‘Watanzania tusikubali kuliingiza taifa kwenye machafuko, kipindi hiki tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na ...

RC MANYARA AWAPONGEZA FRANONE MINING NA CHUSA MINING KWA CSR

Picha
  Na Mwandishi wetu, Mirerani  MKUU wa Mkoa wa Manyara, Queen Cuthbert Sendiga amezipongeza kampuni mbili za Franone mining LTD na Chusa mining LTD kwa kusaidia miradi ya maendeleo katika utekelezaji wa uwajibikaji kwa jamii (CSR) kwenye sekta ya afya mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro. RC Sendiga akizungumza na wamiliki wa migodi ya madini ya Tanzanite kwenye ukumbi wa Mazubu Grand Hotel mji mdogo wa Mirerani, amesema makampuni hayo yanajitoa katika kufanikisha miradi ya maendeleo kupitia utekelezaji wa uwajibikaji kwa jamii (CSR). Ameeleza kwamba kampuni ya Franone mining LTD, imefanya vyema kwani imetenga shilingi milioni 80 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ndani ya ukuta unazunguka migodi ya madini ya Tanzanite. "Pia niishukuru kampuni ya Chusa mining LTD, kwa kujenga wodi ya wanawake na watoto na ofisi ya wauguzi katika kituo cha afya Mirerani," amesema RC Sendiga. Hata hivyo, RC Sendiga amewataka wamiliki wa migodi ya madini ya Tanzanite kushiriki kuchangia shughul...

WAKULIMA WA MPUNGA WATAKIWA KUPIMA AFYA YA UDONGO IGUNGA

Picha
Na Lubango Mleka - Igunga. WAKULIMA wa skimu ya umwagiliaji wa mpunga Mwamapuli, wilayani Igunga, mkoa wa Tabora, wametakiwa kupima afya ya udongo katika mashamba yao ili kuongeza tija na kuendesha kilimo cha kibiashara. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mashine za kisasa za kukoboa na kuvuna mpunga, Grace Nyamwanji, Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wilayani Igunga, amewahimiza wakulima kuanza maandalizi mapema kwa msimu wa kilimo 2025/2026 na kutumia ushauri wa wataalamu wa kilimo.  "Tukipima afya ya udongo, tutapata mavuno bora na kilimo chetu kitakuwa biashara yenye faida," Grace Nyamwanji. Kwa upande wake, Meneja wa Chama cha Ushirika cha Mwamapuli, Nkwabi Igessa, amesema mashine hizo zitasaidia kuongeza uzalishaji, kuleta ajira kwa wananchi na kuongeza mapato ya ushirika huo. Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Sauda Mtondoo, ambaye alikuwa mgeni rasmi, amewataka wakulima kubadilika na kuwekeza zaidi katika kilimo biashara na teknolojia za kisasa ili kuongeza tha...