WAKULIMA WA MPUNGA WATAKIWA KUPIMA AFYA YA UDONGO IGUNGA




Na Lubango Mleka - Igunga.

WAKULIMA wa skimu ya umwagiliaji wa mpunga Mwamapuli, wilayani Igunga, mkoa wa Tabora, wametakiwa kupima afya ya udongo katika mashamba yao ili kuongeza tija na kuendesha kilimo cha kibiashara.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mashine za kisasa za kukoboa na kuvuna mpunga, Grace Nyamwanji, Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wilayani Igunga, amewahimiza wakulima kuanza maandalizi mapema kwa msimu wa kilimo 2025/2026 na kutumia ushauri wa wataalamu wa kilimo.

 "Tukipima afya ya udongo, tutapata mavuno bora na kilimo chetu kitakuwa biashara yenye faida," Grace Nyamwanji.

Kwa upande wake, Meneja wa Chama cha Ushirika cha Mwamapuli, Nkwabi Igessa, amesema mashine hizo zitasaidia kuongeza uzalishaji, kuleta ajira kwa wananchi na kuongeza mapato ya ushirika huo.

Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Sauda Mtondoo, ambaye alikuwa mgeni rasmi, amewataka wakulima kubadilika na kuwekeza zaidi katika kilimo biashara na teknolojia za kisasa ili kuongeza thamani ya mazao yao.

Wakulima wa Mwamapuli wameeleza matumaini makubwa kwamba mashine hizo zitapunguza changamoto walizokuwa wakikumbana nazo awali ikiwemo gharama kubwa na ucheleweshaji wa uvunaji wa mpunga.













📍 Mwamapuli, Igunga - Tabora

🗓️ 24 Oktoba 2025


#Tabora #Igunga #KilimoBiashara #Mwamapuli #Mpunga #Tanzania #Uzalishaji #Ushirika #MaendeleoVijijini




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.