Na Mwandishi Wetu, Iramba. MWANZIRISHI na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya WAZOHURU MEDIA Ndg Mathias Canal amewaongoza Viongozi wa dini, Wadau wa maendeleo na Waumini kwenye harambee ya ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania-KKKT Usharika wa St George Kiomboi Wilaya ya Iramba Mkoani Singida. Katika harambee hiyo iliyofanyika jana tarehe 28 Septemba 2025 katika eneo la Ujenzi wa Kanisa Mtaa wa Lulumba, Mgeni huyo rasmi amesimamia upatikanaji wa fedha taslimu Tsh 79,407,000 ambapo ahadi ni Shilingi Milioni 4,010,000 na jumla ya fedha zote zilizopatikana ni Shilingi Milioni 85,017,000. Mgeni rasmi Ndg Mathias Canal pamoja na marafiki zake waliomuunga mkono amechangia jumla ya Tsh milioni 3,835,000 na mifuko 10 ya Saruji. Akizungumza katika harambee hiyo Mathias amesema kuwa Kanisa ni nguzo muhimu ya maisha ya kiroho, kijamii na hata kiuchumi. Kupitia kanisa waumini wanajifunza misingi ya upendo, mshikamano, uadilifu na ujenzi imara wa taifa. "Ujenzi wa kanisa si kwa aj...