TANZANIA YAENDELEZA USHINDI KATIKA MASHINDANO YA ICC MEN’S T20 WORLD CUP AFRICA QUALIFIER, 2025.

 



Na Mwandishi Wetu,Zimbabwe.

BALOZI wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe. CP. Suzan S. Kaganda, ameongoza maafisa wa Ubalozi kushuhudia Timu ya Taifa ya Cricket ya Tanzania katika mchezo wa mashindano ya ICC Men’s T20 World Cup Africa Qualifier 2025, uliofanyika tarehe 28 Septemba 2025, kati ya Tanzania na Uganda.

Katika mchezo huo uliofanyika kwenye viwanja vya Takashinga vilivyopo mjini Harare, Zimbabwe, Timu ya Taifa ya Cricket ya Tanzania imeibuka mshindi baada ya kuifunga timu ya Uganda kwa runs 9, hatua inayofanya timu ya Tanzania kuendelea na ushindi baada ya kuifunga timu ya Taifa ya Botswana siku ya Ijumaa, tarehe 26 Septemba 2025.

Ushindi huu ni mafanikio muhimu katika ICC Men’s T20 World Cup Africa Qualifier 2025. Kufuatia ushindi huo dhidi ya Uganda, timu ya Tanzania kwa sasa imefuzu kuingia hatua ya nusu fainali.

Mchezo wa nusu fainali utachezwa mnamo tarehe 02 Oktoba 2025, kati ya Tanzania na Namibia kwenye uwanja uliopo mjini Harare, Zimbabwe.

Ubalozi wa Tanzania unaendelea kufuatilia kwa karibu michuano hiyo na kuendelea kuitakia kila la heri Timu ya Taifa ya Cricket ya Tanzania katika mashindano hayo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.