AHSANTE FOUNDATION WACHINJA NG'OMBE KONDOO NA MBUZI EID AL- ADHA MIRERANI
Na Mwandishi wetu, Mirerani. TAASISI ya Ahsante Foundation Tanzania imechinja ng'ombe 723, mbuzi na kondoo 2,500 na kutoa sadaka kwa watoto yatima, wajane, wahitaji na taasisi za serikali na binafsi, katika kusheherekea sikukuu ya Eid Al-Adha mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara. Meneja mipango wa taarifa ya Ahsante Foundation Tanzania, Omary Gyunda amesema lengo ni kuhakikisha jamii yenye mahitaji inanufaika na sadaka ya sikukuu hiyo ya Idd. Gyunda amesema taarifa ya Ahsante Foundation Tanzania wamechinja ng'ombe 723, mbuzi na kondoo 2,500 kwa ajili ya jamii kushiriki sherehe hiyo bila ubaguzi wa madhehebu katika mji mdogo na maeneo ya jirani. Amesema sadaka hiyo ya nyama ya kuchinja imetolewa kwa watoto yatima, wajane, wahitaji mbalimbali na taasisi za serikali na binafsi za mji mdogo wa Mirerani na majirani zao. "Tumetoa sadaka hiyo ya kuchinja kwa wahitaji hao na taasisi mbalimbali ikiwemo shule za msingi, sekondari, polisi, uhamiaji, zimamoto na ...