Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti 18, 2025

TARURA MUSOMA WAPONGEZWA UJENZI WA MIRADI KULINGANA NA THAMANI YA FEDHA.

Picha
Na Mwandishi Wetu, Musaoma.  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Ndugu Ismail Ali Ussi amewapongeza wafanyakazi wa TARURA wilaya ya Musoma kwa kufanya kazi kwa weledi na kuhakikisha wanajenga miradi ya miundombinu ya barabara kulingana na thamani halisi ya fedha. Ndugu Ussi ameyasema hayo wakati akiweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa barabara ya Nyabisarye Mahakama kuu Kanda ya Musoma yenye urefu wa Mita 700 kwa kiwango cha lami . Ussi amesema kuwa Serikali  imekuwa ikitumia fedha nyingi katika ujenzi wa miundombinu ya barabara kwa lengo la kuwarahisishia wananchi huduma katika maeneno yao ili waweze kufanya shughuli zao za kiuchumi na kujiingizia kipato. Kwa upande wake  Kaimu Meneja Wilaya ya Musoma Mhandisi Mohamed Etanga amesema jumla ya shilingi Milioni 600.97 zimetengwa  kwaajili ya ujenzi wa barabara ya Nyabisarye- Mahakama Kuu yenye urefu wa Mita 700 kwa kiwango cha lami . Amebainisha kuwa ujenzi wa barabara hiyo ulianza Oktoba mwaka jana na unatarajiwa kuka...

KILIMANJARO YA SWEDEN YATWAA UBINGWA WA BONANZA LA SERENGETI NCHINI UBELGIJI.

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Ubelgiji.  TIMU ya soka ya Watanzania iitwayo Kilimanjaro kutoka Sweden imetwaa tena kwa mara ya nne mfululizo ubingwa wa kombe la Bonanza la Serengeti katika michuano iliyofanyika tarehe 15-16 Agosti, 2025, jijini Antwerp, Ubelgiji. Kilimanjaro ilitetea ubingwa wake baada ya kuifunga timu nyingine ya Watanzania kutoka Uingereza iitwayo Leeds Swahili mabao 2-1 kwenye mchezo mkali wa fainali. Magoli ya Kilimanjaro yalifungwa na Feisal Amir na Fryad Sabri huku la Leeds likifungwa na Murtaza Fuad. Hii ni mara ya tatu kwa timu hizi kukutana fainali. Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Mhe. Jestas Nyamanga, alimkabidhi kombe la ubingwa nahodha wa Kilimanjaro, Abbas Bachu, ambaye naye alimkabidhi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Mobhare Matinyi, na kuibua shwange za washabiki wao. Kilimanjaro hushiriki ligi ya daraja la sita nchini Sweden katika mfumo wa madaraja saba. Michuano hiyo iliyofanyika kwa mara ya nne tangu mwaka 2021 na kudhaminiwa na Benki ya N...

UMOJA NA MSHIKAMANO VYATAWALA HOTUBA ZA VIONGOZI MKUTANO WA SADC

Picha
Na Mwandishi Wetu, Antananarivo.  MKUTANO wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) umehitimishwa jijini Antananarivo Agosti 17, 2025, huku viongozi hao wakihimizana, umoja, mshikamano na ushirikiano  kama njia ya msingi ya kujikwamua kiuchumi na kukabiliana na changamoto zinazoibuka kila siku ulimwenguni. Katika mkutano huo, Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan aliwakilishwa na Makamu wa Rais, Dkt. Philip Isdor Mpango, na kama ilivyo ada, mwenyeji wa mkutano huo, Madagascar alikabidhiwa uenyekiti wa jumuiya hiyo kutoka Zimbabwe. Mkutano huo ulihudhuriwa na wakuu wa nchi 9 ambapo Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, mwenyekiti aliyopekea kijiti, Katibu Mtendaji wa SADC na wakuu wa nchi wanne wa Botswana, Namibia, Msumbiji na Mauritius kutokana na kushiriki kwao kwa mara ya kwanza kama wakuu wa nchi walipata fursa ya kuhutubia mkutano huo. Hotuba za viongozi hao ziligusia maeneo makubwa manne ambayo ni amani na usalama, ujenzi wa miundombinu, uchumi, demokrasia n...