ZIMAMOTO YAWAKARIBISHA WANANCHI KUPATA ELIMU YA UOKOAJI KATIKA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA
Na Hamida Ramadhan, Dodoma. WANANCHI wametakiwa kutumia fursa ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kutembelea banda la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili kupata elimu ya kujikinga na majanga ya moto pamoja na mbinu za uokoaji wakati wa dharura. Akizungumza katika maadhimisho hayo yanayoendelea jijini Dodoma, Naibu Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Puyo Nzalayaimisi, alisema banda la jeshi hilo limekuwa likitoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kuokoa maisha na mali pindi majanga yanapotokea. Amesema wananchi wanaofika katika banda hilo wanapata mafunzo kuhusu hatua za kuchukua kabla, wakati na baada ya kutokea kwa majanga ya moto pamoja na maafa mengine yanayohitaji huduma za uokoaji. "Tunatumia maonesho haya kukutana moja kwa moja na wananchi na kuwapa elimu itakayowasaidia kujikinga na majanga pamoja na kuelewa namna ya kushirikiana na jeshi la zimamoto wakati wa dharura," amesema. Nzalayaimisi ameleza kuwa elimu hiyo ni sehemu ya mkakati wa jeshi hilo wa ku...