Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi 18, 2026

ZAIDI YA WATOTO 173,255 IGUNGA KUPATIWA CHANJO YA POLIO BAADA YA KIRUSI KUGUNDULIKA JIJINI MWANZA

Picha
  Na Lubango Mleka, Igunga.  Zaidi ya watoto 173,255 wenye umri chini ya miaka kumi wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya ugonjwa wa polio wilayani Igunga mkoani Tabora, kufuatia kugundulika kwa kirusi cha ugonjwa huo mkoani Mwanza. Hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za serikali kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo hatari, hasa kwa watoto wadogo ambao wako kwenye hatari kubwa ya maambukizi. Katika kujiandaa na zoezi hilo, Hospitali ya Wilaya ya Igunga imetoa elimu kwa wadau wa afya kwa lengo la kuwajengea uelewa pamoja na kuongeza nguvu ya uhamasishaji kwa jamii ili kuhakikisha mwitikio unakuwa mkubwa wakati wa utekelezaji wa chanjo hiyo. Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mratibu wa Chanjo wilayani Igunga, Novat Bijana, pamoja na wataalam wengine wa afya, walisisitiza umuhimu wa jamii kujitokeza kwa wingi kuwapeleka watoto kupata chanjo ili kujikinga na madhara ya ugonjwa wa polio. Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Wilaya ya Igunga, Bi. Elizabeth Rwegasila, aliwataka wadau hao kufikisha ...

TANROADS YAPELEKA TABASAMU MWAMGONGO

Picha
Na Allan Kitwe, Kigoma.  WAKAZI wa Kitongoji cha Mgazo, Mtaa wa Lubona katika Kijiji cha Mwamgongo Kata ya Mwamgongo Wilaya ya Kigoma wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuanza kufungua barabara inayoingia kijijini kwao. Wakizungumza mbele ya waandishi wa habari jana wameeleza kuwa tangu nchi ipate uhuru mwaka 1961 Kijiji hicho hakijui usafiri wa barabara kwa sababu kiko kwenye milima na usafiri pekee wanaotegemea ni wa mitumbwi na boti. Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Lubona, Elias Lutaha ameeleza kufurahishwa na hatua ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuipatia TANROADS Kigoma shilingi bilioni 3 kwa ajili ya kuchonga milima na kuanza kufungua barabara hiyo. ‘Tangu tumepata uhuru barabara hii indo imeanza kufunguliwa, kwa sasa ukitoka Kigoma Mjini kupitia Mkongoro unafika katika Kitongoji hiki kwa usafiri wa barabara lakini haifiki Mwamgongo Kijijini’, ameeleza. ‘Barabara yetu imefunguliwa kutoka Chankere hadi hapa Mganzo lakini haifiki Mwamgongo, chonde chonde, Mheshimiwa R...