NAIBU WAZIRI MAKAMBA AIPONGEZA PBPA KWA UTENDAJI KAZI MZURI
Na Mwandishi Wetu - Dar es Salaam Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba (Mb) ameipongeza Wakala ya Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) kwa utendaji kazi mzuri katika kuhakikisha nchi inakuwa na akiba ya mafuta ya kutosha. Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Menejimenti ya PBPA leo jijini Dar es Salaam. "Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya lakini hakikisheni mnatoa elimu kwa Watanzania kuhusu majukumu yenu na kazi zenu" amesema Mhe. Salome. Aidha, ametumia nafasi hiyo kuitaka PBPA kuwawezesha Watanzania wazawa kuingia kwenye biashara ya mafuta na kufanya kazi kwa ushirikiano. "Lazima tupate wawekezaji wa Tanzania, tuwawezeshe waingie kwenye hii biashara " amesisitiza Mhe. Salome. Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala ya Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Bw. Erasto Simon amesema wakala hiyo imefanikiwa kuhakikisha kunakuwa na akiba ya mafuta ya kutosha, uwepo wa takwimu sahihi za kiasi cha mafuta pamoja na kuiwezesha Serikali kupanga ukusanyaji wa mapato. ...