Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti 27, 2025

DKT ASHA -ROSE MIGIRO AMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUMTEUA KUWA KATIBU MKUU WA CCM

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Dodoma KATIBU Mkuu mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt, Asha-Rose Migiro, amemshukuru kwa dhati Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kumuamini na kumteua kushika nafasi hiyo muhimu ndani ya chama. Akizungumza mara baada ya mapokezi hayo katika viwanja vya Makao makuu ya Chama cha Mapinduzi CCM (whitehouse) Dodoma Dkt, Migiro amesema uteuzi huo ni heshima kubwa na dhamana ya kuendeleza misingi ya uongozi wa chama, huku akiahidi kutekeleza majukumu yake kwa weledi, bidii, na uaminifu mkubwa. “Ninatoa shukrani za dhati kwa Mwenyekiti wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuniamini na kunipa jukumu hili ni heshima kubwa kwangu, na naahidi kulitumikia chama chetu kwa moyo wangu wote,” amesema Dkt. Migiro. Aidha amewataka wanachama hao kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu unaotaraji kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.  Pmoja na haya amewashukuru wanachama wa CCM kwa mapokezi mazuri aliyoyapata, akisema kuwa ni ishara ya mshi...