MBUNGE MNZAVA AWAKABIDHI WAZEE 300 BIMA ZA AFYA KUPITIA MAKUYUNI FESTIVAL
Na Mwandishi Wetu, Korogwe. MBUNGE wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Mhe. Timotheo Mnzava, ameendelea kutekeleza mikakati ya kuboresha huduma za afya kwa wazee kwa kugawa Bima za Afya kwa zaidi ya wazee 300 waliohudhuria Makuyuni Festival, tamasha lililowakutanisha wakazi wa maeneo mbalimbali ya jimbo hilo. Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mhe. Mnzava amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha wazee wanapata huduma bora za matibabu bila vikwazo vya kifedha, huku akisisitiza kuwa afya ya wazee ni sehemu muhimu ya ustawi wa jamii. "Bima hizo zitawawezesha wazee kupata matibabu kwa wakati wowote na katika vituo vilivyosajiliwa, hatua inayotafsiriwa kama kupunguza mzigo wa gharama za afya kwa familia nyingi za kipato cha chini."amesema Mhe.Mnzava Katika tamasha hilo, Mbunge Mnzava pia alipata fursa ya kushiriki chakula cha pamoja na wazee, watu wenye ulemavu, vijana na wananchi wengine waliohudhuria, akisema kitendo hicho ni sehemu ya kuimarisha mshikamano na kuonyesha ushiriki...