Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi 9, 2026

WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI SHULE YA AMALI MKOANI RUKWA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Rukwa.  WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Jumatatu, Machi 9, 2026 ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Amali ya Mkoa wa Rukwa iliyopo katika Kata ya Majengo, Namanyere, Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa. Mradi huo unatekelezwa kupitia Programu ya Kuboresha Ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) kwa gharama ya shilingi bilioni 1.6 na unalenga kuboresha elimu ya ufundi stadi kwa kuwaandaa wanafunzi kupata ujuzi utakaowawezesha kujiajiri na kuchangia maendeleo ya kiuchumi ya Taifa. Mradi huo ulianza kutekelezwa Desemba 20, 2024 na ulitarajiwa kukamilika Machi 30 2025, ambapo hadi sasa jumla ya shilingi bilioni 1.5 zimetumika katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za ujenzi wa miundombinu ya shule hiyo. Kwa mujibu wa taarifa ya mradi, hadi sasa ujenzi wa madarasa nane pamoja na jengo la utawala umekamilika na miundombinu hiyo tayari inatumika. Pia ujenzi wa jengo la TEHAMA na maktaba, nyumba ya mtumishi pamoja na vyoo vya wavulana na w...

DKT. MWIGULU: WANAFUNZI WATAKAOFAULU VIZURI KUSOMESHWA NJE YA NCHI KUPITIA SAMIA SCHOLARSHIP

Picha
  Awafikishia wanafunzi salamu za Rais Dkt. Samia; asema Serikali inaendelea kuwekeza katika elimu Na Mwandishi Wetu, Rukwa.  WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema wanafunzi watakaofaulu kwa viwango vya juu watanufaika na ufadhili wa masomo kupitia mpango wa Samia Scholarship unaotolewa na Serikali. Dkt. Mwigulu amesema hayo wakati akizungumza na wanafunzi katika ziara yake mkoani Rukwa, ambapo pia aliwasilisha salamu maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan. “Daktari Samia Suluhu Hassan anasema kwa wale watakaofaulu kwa kiwango cha juu wanapata ufadhili asilimia 100. Na sio ufadhili tu wa asilimia 100 peke yake, asilimia 100 na unaenda kusoma nchi yoyote duniani… hiyo inaitwa Samia Scholarship,” alisema Waziri Mkuu. Aidha, alisema Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika sekta ya elimu ambapo zaidi ya shule za sekondari 1,300, shule za msingi zaidi ya 2,700 pamoja na maelfu ya madarasa yamejengwa ka...

DKT. MWAMBA: TUMIENI JUKWAA LA WANAWAKE NA KODI KUTOA ELIMU

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam.  KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba amewataka Wanawake wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kutumia Jukwaa la Wanawake na Kodi lililozinduliwa  hivi karibuni kuelimisha wajasiriamali wanawake kuhusu umuhimu wa kujisajili, kuwasilisha taarifa sahihi na kulipa kodi kwa wakati. Dkt. Mwamba ametoa wito huo wakati akizungumza na wanawake wa TRA,  katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam. Sherehe hizo zilihudhuriwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Juma Mwenda, Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Mcha Hassan Mcha, Kaimu Mkurugenzi Usimamizi Rasilimali watu na Utalawa Bw. Nahoda Pandu Nahoda.

PROF. KABUDI AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA 26 WA MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE WA JUMUIYA YA MADOLA

Picha
  Na Mwandishi Wetu, London.  WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Palamagamba J. Kabudi, ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 26 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Madola (CFAMM) uliofanyika Machi 8, 2026 jijini London, Uingereza akimwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb). Akichangia mjadala, Prof. Kabudi amesema Jumuiya ya Madola inapaswa kubaki kuwa jukwaa muhimu la kushughulikia changamoto za maendeleo na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa (multilateralism) katika kipindi cha sasa chenye changamoto za kisiasa, kiuchumi na kimazingira. Katika masuala ya uchumi, Prof. Kabudi amesisitiza umuhimu wa kuimarisha biashara na uwekezaji kati ya nchi wanachama kwa kujifunza kutoka mifano ya ushirikiano wa kikanda kama Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA). Amesema jukwaa la biashara na uwekezaji la Jumuiya ya Madola litasaidia kupunguza vikwazo vya biashara na kuongeza biashara kati ya ...

e-GA YATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE UHUTAJI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Pwani.  KATIKA kuadhimisha kilele cha Siku ya Wanawake Duniani, inayoadhimishwa kila mwaka Machi 8, wanawake wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) wametoa msaada wa mifuko 50 ya saruji, matofali 1,000 pamoja na mahitaji mbalimbali ya watoto katika Kituo cha kulea watoto yatima na waliofanyiwa ukatili cha Shalom kilichopo Kidenge B, Kata ya Msangani, Halmashauri ya Mji wa Kibaha, mkoani Pwani Machi 6, 2026. Akizungumza jana wakati wa kukabidhi msaada huo, Meneja wa Udhibiti na Viwango wa Mamlaka hiyo Bi. Sultana Seiff, alisema kuwa wanawake wa e-GA wameamua kusherehekea siku hiyo kwa kuwafikia watoto wanaohitaji msaada katika jamii na kukichagua kituo hicho ikiwa kama sehemu ya kurudisha kwa jamii. Meneja huyo alisema kuwa baada ya kuwasiliana na kituo hicho na kupata changamoto mbalimbali zinazohitaji kutatuliwa katika kituo hicho ikiwemo ujenzi wa uzio ili kuhakikisha Watoto hao wanakua salama waliamua kuchangia vifaa vya ujenzi pamoja na mahitaji mengine muhimu...