DKT. MWAMBA: TUMIENI JUKWAA LA WANAWAKE NA KODI KUTOA ELIMU




Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam. 

KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba amewataka Wanawake wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kutumia Jukwaa la Wanawake na Kodi lililozinduliwa  hivi karibuni kuelimisha wajasiriamali wanawake kuhusu umuhimu wa kujisajili, kuwasilisha taarifa sahihi na kulipa kodi kwa wakati.

Dkt. Mwamba ametoa wito huo wakati akizungumza na wanawake wa TRA,  katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

Sherehe hizo zilihudhuriwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Juma Mwenda, Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Mcha Hassan Mcha, Kaimu Mkurugenzi Usimamizi Rasilimali watu na Utalawa Bw. Nahoda Pandu Nahoda.











Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.