Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni 24, 2026

WANANCHI WAHIMIZWA KUTUMIA LANDMAX KUEPUKA UTAPELI WA ARDHI

Picha
   Na Hamida Ramadhan,Dodoma MBUNGE wa Jimbo la Mbozi, Onesmo Mnkondya, amewataka wananchi na madalali wanaohusika na biashara ya ardhi kutumia huduma za Landmax Real Estate Company Limited ili kufanya uwekezaji kwa usalama na kuondokana na migogoro inayotokana na mauzo au ununuzi usio rasmi wa ardhi. Mnkondya, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Landmax Real Estate Company Limited, amesema hayo Juni 24, 2026 jijini Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa ofisi za kampuni hiyo. Amesema Landmax imeanzishwa kwa lengo la kuwasaidia wananchi kupata ardhi salama na makazi bora huku ikichangia kupunguza migogoro ya ardhi. Aidha, amebainisha kuwa kampuni hiyo inatoa huduma mbalimbali ikiwemo uuzaji na ununuzi wa ardhi na mali isiyohamishika, ushauri wa uwekezaji wa ardhi, usimamizi wa mali, urasimishaji wa nyaraka za ardhi, uendelezaji wa miradi, tafiti za soko pamoja na ushirikiano katika miradi ya maendeleo. “Tunawaalika wananchi na madalali wote wanaotaka kununua au kuuza ardhi kufika ofisi...

RC MTANDA AWATAKA MISUNGWI DC KUSHIRIKIANA KUWALETEA MAENDELEO WANANCHI

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Mwanza.  MKUU wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameitaka halmashauri ya wilaya ya Misungwi kuimarisha umoja baina ya Baraza la Madiwani na Menejimenti kuwaletea wananchi huduma bora za kijamii kwa kutumia mapato ya ndani kwa kujenga shule, vituo vya afya na miundombinu ya maji. Mhe. Mtanda amefikia hatua ya kutoa agizo hilo baada ya kubaini uwajibikaji duni kwenye ukusanyaji kwa mwenendo wa miaka mitatu na udhaifu kwenye kujibu hoja ambapo kwa mwaka husika wa fedha hoja 81 zimetekelezwa 23 pekee sawa na asilimia 28.4 huku hoja 57 bado hazijajobiwa sawa na asilimia 70.4. Ametoa agizo hilo leo tarehe 24 juni, 2026 wakati akihutubia Mkutano Maalumu wa Baraza la Madiwani wa kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na Maagizo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC) 2024/25 ambapo wamepata hati safi. "Maendeleo ya Misungwi yanawategemea ninyi viongozi na watendaji mlioaminiwa hapa, mkileta mzaha kwenye uwaji...

RC MTANDA AIAGIZA KWIMBA DC KUTUMIA MAPATO YA NDANI KWA MIRADI YA KIMKAKATI

Picha
  Na Mwandishi Wetu, Mwanza.  MKUU wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewapongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba kwa kufikia malengo kwenye ukusanyaji wa mapato kwa kipindi cha miaka minne mfululizo ambapo amewataka kutumia mapato hayo kujenga miradi mikubwa ya kimkakati. Ametoa agizo hilo leo tarehe 24 juni, 2026 wakati akihutubia Mkutano Maalumu wa Baraza la Madiwani wa kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na Maagizo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC) 2024/25 ambapo wamepata hati safi. Mhe. Mtanda amesema ni wakati sasa kwa halmashauri kuwekeza kwenye miradi mikubwa ambayo italeta makusanyo makubwa zaidi na kuongeza wigo wa ukusanyaji mapato badala ya kujenga miradi mingi midogo pekee ambayo kimsingi haitumiki kurejesha fedha. "Tumieni asilimia 40 ya makusanyo yenu kwa mujibu wa sheria kufanya hata mradi mmoja mkubwa ambao utakuwa alama kama wa uwanja wa mpira ambao mtajihakikishia ukusanyaji wa mapato kwa siku...