MBOSO ATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA ILEMELA.



Na Mwandishi Wetu, Ilemela - Mwanza. 

MSANI wa kizazi kipya Mbwana Yusuph Kilungi (Mbosso) amefika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe Amir Mkalipa kwa ajili ya kujitambulisha na pia kufanya tendo la hisani kwa kutoa msaada kwa kituo cha Hisani ambacho kinahudumia watoto yatima na wenye mahitaji maalum kilichopo wilayani hapa

Mhe Mkalipa akimkaribisha msanii huyo, alitumia wasaa huo kumueleza fursa mbalimbali zilizopo wilayani hapa lakini pia kumshauri juu ya kuwekeza kwani wakati ni sasa.

Mbisso akiwa katika kituo cha hisani ameweza kula chakula cha mchana na watoto hao na ametoa misaada mbalimbali ikiwemo magodoro, chakula, vyandarua n.k, lakini pia ameahidi kuchangia bima ya afya ya watoto hao.





Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.