IGUWASA YAUNGA MKONO JITIHADA ZA RAIS, DKT. SAMIA KWA KUPANDA MITI.

 


Tabora, Januari 27, 2026.

Na Lubango Mleka, Igunga.

KAATIKA kuunga mkono tamko la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuhusu upandaji wa miti kama sehemu ya utunzaji wa mazingira, Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Wilaya ya Igunga (IGUWASA) imefanya zoezi la upandaji wa miti mbalimbali katika eneo la ofisi zake.

Zoezi hilo limefanyika ikiwa ni kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya Mheshimiwa Rais, ambapo taasisi hiyo imeeleza kuwa inalenga kuhamasisha jamii kushiriki kikamilifu katika kulinda na kuhifadhi mazingira kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho.

Viongozi na watumishi wa IGUWASA wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Bi. Selwa  Abdallah Hamid wameshiriki katika zoezi hilo, wakisisitiza kuwa upandaji miti ni hatua muhimu katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kuhakikisha upatikanaji endelevu wa rasilimali za maji.

IGUWASA imewahimiza wananchi kuiga mfano huo kwa kupanda na kutunza miti katika maeneo yao ili kuunga mkono jitihada za serikali katika uhifadhi wa mazingira.










Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.