HALMASHAURI YA IGUNGA YAUNGANA NA WATANZANIA KUPANDA MITI
Na Mwandishi Wetu, Igunga.
MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Selwa Hamid ameiongoza Menejimenti ya Halmashauri hiyo kupanda miti kwa lengo la kuitekeleza 27 ya kijani iliyoasisiwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.
Selwa ameungana na viongozi hao leo, ikiwa ni ishara ya kuendelea kumuunga mkono Rais Dk. Samia katika kumbukizi ya kazaliwa kwake.
"Kipekee ninaishukuru na kuipongeza Menejimenti kujindaa na kushiriki zoezi hili baada ya masaa ya kazi kuungana na 27 ya kijani ikiwemo kumpongeza na kumtakia kila la kheri Mheshimiwa. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan," ameshukuru.
Ameeleza kuwa wamepanda miche 70 ambapo miche 50 yakivuli huku 20 ikiwa ni ya matunda ambayo yatawafaidisha vizazi na vizazi.






Maoni