TIMU YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAMTEMBELEA MDAU WA UTALII MZEE GEOFF FOX.
Na Lubango Mleka, Iringa.
TIMU ya Wataalamu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii ikiongozwa na Mkurugenzi Msaidizi, Bi. Dainess Kunzugala leo Novemba 19,2025 imemtembelea mdau mkubwa wa utalii na uhifadhi kwa Kanda za Nyanda za juu Kusini Mzee Geoff Fox wilayani Mufindi mkoani Iringa lengo ikiwa ni kumhamasisha kuingia katika kuwania tuzo za uhifadhi na utalii za Serengeti 2025.
Mzee Fox anamiliki kambi za kitalii (lodges) 7 ndani ya hifadhi na ndiye mwanzilishi wa Hifadhi ya Taifa ya Saadani.
Aidha, Mzee Fox ni mwekezaji wa kwanza wa kambi ya utalii katika Hifadhi ya Taifa Ruaha na ni kinara katika uhifadhi kwa kutunza na kulinda miti ya asili.


Maoni