USINDI AMCOS WANUNUA TREKTA KWA KILIMO NA KUJIONGEZEA KIPATO

 


Na Lubango Mleka, Kaliua.

CHAMA Cha Msingi Usindi AMCOS Ltd cha Kaliua Mkoani Tabora kimenunua Trekta kwa ajili ya kufanyia shughuli za Kilimo na pia watakodishia kufanyia shughuli za Kiuchumi kujiongezea kipato.

Uzinduzi wa Trekta umefanywa Desemba 23, 2025 na Katibu Tawala Wilaya ya Kaliua Sosthenes Chakupanyuka, katika Mkutano Mkuu wa kufunga mwaka wa Chama hicho.

Sosthenes amewapongeza kwa hatua hiyo kubwa na kusema Usindi AMCOS ni chama cha mfano wa kuigwa kwa Kaliua kwa kutimiza vyema lengo lao la kununua Trekta yao ya pili.Ameahidi kuwa nao pamoja  penye changamoto ashirikishwe.

Pia amefurahishwa sana na namna ambayo wamekuwa wakijali jamii kwani wameweza kutoa mifuko 100 ya Simenti kwa ajili ya kujenga shule, kuweka umeme kwenye shule za Msingi na kujenga barabara ya kuelekea Zahanati ya Usindi.

Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Tabora Venance Msafiri ameahidi kuwapeleka wakulima mafunzo kuongeza Elimu ya Kilimo na Madereva wa Matrekta kuongeza ujuzi. 

Msafiri amewapongeza Usindi AMCOS kwa kupata Hati Safi kwani  ni miongoni mwa Vyama vichache vilivyoweza kufika hatua hiyo.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.