MAMBO YALIYOJIFICHA KUHUSU HIFADHI YA TAIFA YA MILIMA UDZUNGWA

 











1. Hifadhi ina njia mbalimbali za matembezi ya miguu na jumla ya Maporomoko ya maji 6 (Sanje, Sonjo, Njokamoni, Prince Benhard, Ichonde na Mwaya).

2. Vilele vikubwa vya  Milima (Luhomero mita 2,576  na Mwanihana mita 2,500 kutoka usawa wa bahari).

3. Kitovu cha Viumbe Adimu. Udzungwa ina viumbe wengi adimu ambao huwezi kuwapata mahala popote duniani. Spishi hizo ni pamoja na jamii mbili za primata (Ngolaga wa Sanje na Mbega wekundu wa Iringa), Spishi 2 za ndege (Kware wa Milima ya Udzungwa na “Rufous-winged Sunbird), Spishi 4 adimu za mimea ambapo moja wapo ni “Vernonia luhomeroensis”, Spishi 3 za vipepeo ambazo ni pamoja na “Charaxes lucyae mwanihanae”, Spishi ya Nyoka aitwaye “Red Snouted Wolf Snake na viumbe wengine wengi.

4. Baadhi ya Spishi nyingine adimu zinapatikana katika Milima ya Tao la Mashariki (Eastern Arc Mountains) baadhi ya spishi hizo  ni pamoja na Kinyonga Mfupi (Pygmy Chameleon).










 #UdzungwaNountainsNationalPark #HikingParadise #tanzaniaparks

#UtaliiwandanihifadhiyataifamilimaUdzungwa

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.