ADEN AAHIDI MAKUBWA DODOMA.
Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
MWENYEKITI wa Chama cha Soka Mkoa wa Dodoma (DOREFA) Aden Mohammed ameahidi makubwa zaidi kwa soka la Mkoa wa Dodoma ikiwemo kuweka mazingira rafiki kwa klabu zinazoutumia uwanja wa Jamhuri kama uwanja wa nyumbani.
Aden ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF na Mjumbe wa Kanda namba 4 inayojumisha Mikoa ya Singida,Dodoma,Shinyanga na Simiyu amesema wanafurahi kwa jinsi ambayo Mkoa wa Dodoma umekuwa na timu nyingi za Ligi Kuu,Dodoma Jiji,Mtibwa Sugar na Tanzania Prisons.
Amesema Dorefa itaendelea kuweka mazingira rafiki na wezeshi ili klabu hizo ziendelee kuutumia uwanja wa Jamhuri kama uwanja wa nyumbani kwa kuhakikisha zinafanya vizuri.
"Niwaahidi wana Dodoma, Dorefa itaendelea kuhakikisha soka linachezwa kuanzia ngazi ya chini mpaka ya juu lengo vipaji vizidi kuonekana,"amesema Aden.




Maoni