WANAFUNZI WA VYUO VIKUU NA KATI WATAKIWA KUTUMIKIA JAMII KWA KUJIFUNZA SHERIA NA KUTOA MSAADA WA KISHERIA.



Na Jasmine Shamwepu Dodoma 

WANAFUNZI wa vyuo vikuu na vyuo vya kati nchini wametakiwa kujitoa kwa ajili ya kutumikia jamii kwa kujifunza sheria na kutoa msaada wa sheria kwa wananchi ili kukabiliana dhidi ya dhulma, uonevu, ukatili wa kijinsia, na migogoro ya ardhi inayoongezeka kila kukicha.

Akizungumza katika Mdahalo  maalum lililofanyika katika Ukumbi wa Chimwaga uliopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma, Mkurugenzi wa Huduma  za msaada wa Sheria  Ester Msambazi  kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, amesema watu wengi wanapoteza haki zao nchini kwa kutojua sheria. 

Msambazi amesema lengo la Mdahalo huo ni kuwajengea uwezo wanachuo hao kuelewa masula ya kisheria na kutambua haki zao pamoja na kufahamu wapi pa kupata huduma za msaada wa kisheria wanakupambana na changamoto."

"Wizara ya katiba na sheria una Jukumu la kratibu na kusimamia upatikanaji wa haki nchini hivyo inaendelea kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo Tehama ili kuhakikisha HUDUMA hizo zinawafikia wananchi wengi zaidi"Amesema

Naye Dkt. Elia Mwanga  wa Shule Kuu ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Dodoma, amesema licha ya kuwepo changamoto mbalimbali chuoni hapo, chuo kinajitahidi kufundisha kwa weledi ili kuzalisha wahitimu watakaoweza kupunguza mrundikano wa kesi za madai na jinai nchini.

Pia, Mkurugenzi wa tehama  TEHAMA katika Mahakama Kuu nchini, Enock Kalege amesema wanawake wengi wanakumbana na udhalilishaji mitandaoni ikiwemo kuvujishwa kwa video zao za faragha lakini hawana uelewa wa taratibu za kisheria zitakazoweza kuzuia na kutokomeza uhalifu huo.

Kongamano hilo lilihudhuriwa na mwanasheria mbobevu, Dkt Godfrey Chambua ambaye ametoa elimu ya namna ya kutatua migogoro kwa njia za jadi zilizokwepo kabla ya ukoloni ili kumaliza migogoro kwa wepesi na kudumisha uhusiano mwema, amani, na utulivu.

Takriban wanafunzi 2000 wameshiriki Mdahalo huo ambapo wameshukuru kwa kupata elimu nzuri huku wakiahidi kujitolea kusaidia jamii pindi watakapohitimu masomo yao.











Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.