MWENYEKITI WA BODI YA ARAB CONTRACTORS AKAGUA MRADI WA BWAWA LA JULIUS NYERERE.
Mwenyekiti wa Bodi ya Arab Contractors akagua Mradi wa Bwawa la "Julius Nyerere" Nchini Tanzania Kuimarisha Ushirikiano kati ya Misri na Tanzania.
MHANDISI Ahmed Al-Assar, Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Arab Contractors, na Mhandisi Wael Hamdy, Naibu Mwenyekiti wa Elsewedy Electric Group, wamefanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa bwawa na kituo cha umeme cha Julius Nyerere nchini Tanzania, unaotekelezwa na makampuni hayo mawili ya Misri kwa ushirikiano na serikali ya Tanzania.
Ziara hii inakuja kama sehemu ya juhudi za kuimarisha mahusiano kati ya Misri na Tanzania, na kufuatilia utekelezaji wa mradi huu mkubwa unaoonesha ukina wa ushirikiano kati ya mataifa haya mawili na dhamira ya Misri ya uungaji mkono juhudi za maendeleo barani Afrika, hasa katika sekta za miundombinu na nishati.
Mradi huu ni miongoni mwa miradi mikubwa zaidi barani Afrika, wenye lengo la kuzalisha megawati 2115 za umeme na kudhibiti mafuriko ya Mto Rufiji, jambo litakalochangia kulinda mazingira na kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa ajili ya kilimo, uvuvi na maisha ya wanyamapori.
Aidha Mradi huu umetengeneza fursa za ajira kwa zaidi ya wafanyakazi 1900, wengi wao ni Watanzania, na unaonesha uwezo wa makampuni ya Misri katika kutekeleza miradi mikubwa inayounga mkono maendeleo endelevu nchini Tanzania na pia, inaimarisha nafasi ya Misri kama mshirika wa kimkakati kwa ndugu wa kiafrika.
CHANZO ni Nasser International forum.


Maoni