TANZANIA NA KENYA KUONDOA VIKWAZO VISIVYO VYA KIUSHURU KUIMARISHA BIASHARA.








Na Mwandishi Wetu, Dar Es Salaam.

TANZANIA na Kenya zimeahidi kuendelea kuondoa vikwazo visivyo vya kiushuru katika biashara baina yao na kuvigeuza kuwa fursa za kukuza uchumi. 

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara wa Tanzania, Dkt. Hashil Abdallah, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 9 wa Kamati ya Pamoja ya Biashara uliofanyika Dar es Salaam. 

Amesema biashara ndiyo msingi wa mahusiano kati ya nchi hizo, kupitia kuongeza ajira, kujenga viwanda na kuhamasisha ubunifu wa wajasiriamali ili kuboresha maisha ya wananchi.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Biashara na Viwanda ya Kenya, Bi. Regina Ombam, amesema Kenya na Tanzania zina mahusiano ya kihistoria, kitamaduni na kiuchumi.

Huku akibainisha kuwa, uchumi wa Tanzania unaendelea kukua kwa kasi hasa katika sekta za viwanda, ujenzi na utalii,  jambo linalofungua fursa kubwa kwa wafanyabiashara na wawekezaji wa Kenya. Aidha, amesisitiza kuwa nchi hizo mbili si majirani tu, bali ni mataifa ya kindugu na wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yenye dira ya mshikamano, ustawi na amani.




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.