NKINGA HOSPITALI YAOKOA MAISHA YA MAMA ALIYEPATA TATIZO LA KUJIFUNGUA

 


Na Mwandishi Wetu, Nkinga - Igunga. 

IDARA ya Wanawake na Uzazi katika Hospitali ya Rufaa ya Nkinga imefanikiwa kuokoa maisha ya bi. Mbalu Jisinza (45), mkazi wa kijiji cha Mwanzugi wilayani Igunga, aliyepata tatizo hatari la kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua, hali iliyohatarisha maisha yake kabla ya kupatiwa matibabu ya haraka na ya kibingwa hospitalini hapo.

Akizungumza wakati anapatiwa matibabu Hospitalini hapa Bi.Jisinza amesema, anachokumbuka mara ya mwisho alikuwa kwenye kituo cha afya kwaajili ya kujifungua, ambapo alijifungua mtoto mfu kisha akaanza kutokwa na damu nyingi, juhudi za madaktari kuzuia  tatizo la kutokwa na damu zilishindikana wakamfanyia upasuaji wa kuondoa kizazi, lakini bado damu zilikuwa zinatoka.

Akiwa kituoni hapo alianza kushindwa kupumua wakamuwekea mpira wa Oxygen akiwa hajitambui, alipata fahamu akiwa chumba cha (ICU) hapa Nkinga Hospitali, Bi.Mbalu amewashukuru madaktari na Wauguzi wa Nkinga Hospitali kwa huduma nzuri waliyompatia tangu wamempokea kwani sasahivi anaendelea vizuri. 

Dkt.Malimi Ngissa ni Daktari toka idara ya Wanawake na Uzazi amesema, bi.Mbalu alipata changamoto ya kutokwa na damu nyingi (PPH) akiwa kituoni hapo. Ambapo hadi Madaktari wetu wanafika kwaajili ya kutoa msaada alikuwa ameongezewa chupa 8 za damu.

Madaktari wa Nkinga Hospitali walifanikiwa kuzuia changamoto ya kutokwa na damu baada ya kumfanyia Upasuaji mwingine tumboni ukiwa ni upasuaji wake 3, baadae alionekana kuwa na changamoto iliyosababishwa na upasuaji, kwani alikuwa akivuja mkojo tumboni baada ya Kibofu kupata shida.

Walimpa rufaa kuja Hospitalini Nkinga kwaajili ya matibabu zaidi ya kibofu cha mkojo ambapo alikaa ICU kwa siku 4  kutokana na hali mbaya aliyokuwanayo.

Dkt.Ngissa amewahimiza Wanawake kupenda kuhudhuria Kliniki kwa uaminifu na kufanyia kazi ushauri wanaopewa na wataalamu wa afya ikiwemo kujifungulia Hospitali kubwa kwa walio na vidokezo vya hatari kama vile uzao zaidi ya nne na kuendelea.

Kwakuwa afya ya mama na mtoto ndio kipaumbele cha Hospitali ya Rufaa ya Nkinga, mara zote taasisi hii imekuwa tayari kutoa msaada wa haraka pale inapohitajika katika Hospitali za Wilaya, Vituo vya Afya na Zahanati.







Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.