IGP CAMILLUS WAMBURA AFUNGA RASMI MAFUNZO YA AWALI YA ASKARI POLISI KOZI NO:1/2024/2025 CCP MOSHI.
Na Lubango Mleka, Moshi.
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura, leo Novemba 21,2025 amefunga rasmi Mafunzo ya Awali ya Askari Polisi Kozi No: 1/2024/2025 katika Shule ya Polisi Moshi Kilimanjaro.
Akifunga mafunzo hayo IGP Wambura, amewataka askari wahitimu kwenda kutekeleza kwa vitendo yale waliyojifunza kwa kuhakikisha wanaimarisha usalama wa raia na mali zao kwa kudhibiti vitendo vya kihalifu.
IGP Wambura, ameendelea kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kutoa ajira ndani ya Jeshi la Polisi pamoja na mambo mengine ikiwemo suala la kuimarisha miundombinu.
Jumla ya wahitimu 4826 wakiwemo wapiga buruji wamehitimu mafunzo hayo ya awali yaliyodumu kwa muda wa miezi kumi na mbili na askari hao wahitimu wamejengewa uwezo katika maeneo mbalimbali ya kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unaendelea kuimarika nchini.









Maoni