MAONYESHO YA NANE NANE KANDA YA ZIWA MAGHARIBI 2025 YAFUNGULIWA RASMI








Na Lubango Mleka, Mwanza.

MGENI rasmi Mhe. Hashimu Abdallah Komba, Mkuu wa Wilaya ya Geita akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Geita Ndg. Martin Shigela leo tarehe 03 Agosti 2025, amefungua rasmi maonesho ya Nanenane kanda ya ziwa Magharibi yanayofanyika viwanja vya Nyamhongolo Wilaya ya Ilemela ambapo amesema kila mmoja anao wajibu wa kutembelea maonesho haya ya nane nane kwa ajili ya kujifunza lakini pia kujioatia bidhaa mbalimbali. 

“Kama ni mkulima utapata fursa ya kujifunza kilimo cha kisasa na Chenye tija na kama ni mvuvi pia unaweza kujifunza shughuli za uvuvi kwa teknolojia ya kisasa hivyo msiache kutembelea mabanda mbali mbali kujipatia elimu na uzoefu ” Alilisitiza muwakilishi huyo wa mgeni rasmi Mhe Komba. 




Akifafanua kauli mbiu ya maonyesho ya Nanenane Mwaka huu “Chagua viongozi bora kwa maendeleo endelevu ya kilimo, mifugo na uvuvi 2025” amewataka wananchi kushiriki uchaguzi mkuu kwa amani na utulivu na kuchagua viongozi bora watakaowaletea maendeleo.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MWENYEKITI NAMALULU AWEKWA PEMBENI KUPISHA UCHUNGUZI

IGUNGA YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA NANENANE TABORA.